Mapendekezo kwa Sekretarieti ya Ajira

Mapendekezo kwa Sekretarieti ya Ajira

WISE BOY

JF-Expert Member
Joined
Dec 26, 2011
Posts
782
Reaction score
244
Tunashukuru kwa kazi ambayo sekretarieti ya ajira wamekua wakiifanya, japo mapungufu yapo lakini pia wamesaidia ajira za serikalini kufahamika wazi panapokua na uhitaji.
Lakini ingependeza zaidi kama pangekuwepo na chombo huru ambacho kinaikagua sekretarieti katika utendaji na utekelezaji wa shughuli zake; ili kuhakikisha taratibu, sheria na kanuni zinafuatwa. Chombo hiki pia kipewe mamlaka ya kusikiliza malalamiko yenye mashiko kwa watu ambao hawajaridhika na utendaji wa sekretarieti katika jambo flani au kwa ujumla, na kutengua maamuzi ya sekretarieti pale inapobidi, maana kadiri siku zinavyo songa mbele weledi wa sekretarieti unaonekana kushuka na inaonekana kufanya kazi kwa mazoea.
Hii itasaidia kuboresha mfumo wa ajira nchini hasa kupitia kwa sekretarieti na kupunguza madhaifu ambayo yamekua yakiumiza na kusikitisha sana haswa kwa "watoto wa wakulima".
Narudia tena kuishukuru na kuipongeza sekretarieti katika yale iliyofanikisha, na kwa yale madhaifu naamini uwepo wa chombo hicho utayapunguza.
Nawasilisha.
 
Nijuavyo mimi Kila taasisi ya serikali ina kamati ya malalamiko. Kamati hii hushugukia malalamiko ya Ndani Na nje pia,halafu humjibu mlalamikaji hatua ambazo zimechukuliwa kutatua lalamiko husika

Sitaki kuamini kama Hawa jamaa hawana hii kamati maana kwa nature ya Kazi yao hii kamati muhimu sana.
 
Mkuu kama ipo itakua ya ndani, ambayo mara zote huwa si huru. Sijaona chombo huru chochote cha juu kinacho watazama na kusikilza malalamiko
 
Upo sahihi ni chombo cha ndani na kwa utaratibu kinatakiwa kiwe huru na kuripoti kwa mkuu wa taasisi husika

Mkuu wasiwasi wangu ni kuwa na utitiri wa vyombo huru ambavyo vinatumia pesa ya uma bila kuleta tija yoyote. Kwa Maana hiyo mimi Naona ni boraa kukipa makali chombo Cha ndani kwa kutumia policy za ndani kuliko kuanza kuunda kipya
 
kwanza ninamika kibao naomba kazi utumishi hawajawahi niita kwenye usahili hapa najiluiza ivi nii tatizo?cv yangu mbovu, sio tosherezi au tatizo kitu gani......japo hakuna uwioano mzuri wanapoita watu kwenye usahili i mean watuwa wanakuwa kibao niltaniitwe tu nami nioneshere uwezo wangu.
 
Jitahidi kufuata maelekezo kama kuandika kazi na taasisi iliyopo hiyo nafasi
 
Upo sahihi ni chombo cha ndani na kwa utaratibu kinatakiwa kiwe huru na kuripoti kwa mkuu wa taasisi husika

Mkuu wasiwasi wangu ni kuwa na utitiri wa vyombo huru ambavyo vinatumia pesa ya uma bila kuleta tija yoyote. Kwa Maana hiyo mimi Naona ni boraa kukipa makali chombo Cha ndani kwa kutumia policy za ndani kuliko kuanza kuunda kipya

Wazo lako ni zuri mkuu... japo chombo cha ndani kuwa huru sidhani kama ni jambo rahisi sana
 
nimeyafuata hayo yote ndugu yangu lakini hapana sikui itwa....may be bahati yangu haijafika.
 
Huo ni ukweli usiopingika,sekretarieti ya ajira imepoteza kabisa dhamira yake kwa sasa,Nina ushahidi wa kutosha jinsi Mashirika na Taasisi za serikali zinavyotoa shinikizo kwa chombo hiki juu ya wakina nani wanatakiwa waajiliwe.Mfano usaili uliofanyika hivi karibuni wa Tanroads.
 
kumbe usaili wao ni kiini macho.
 
Tupe uzoefu mkuu wamefanya nn kwenye huo usaili wa tanroads ?
 
Braza nachotaka kukushauri zaidi usiweke sana matumaini kwa hawa jamaa,zamani kidogo walikuwa sahihi,lakini siku hizi wanaingiliwa sana na mashirika na taasisi za serikali has a zile zenye maslahi mazuri,watu wanataka waweke legacy ya watoto wao maofisini.
 
kumbe usaili wao ni kiini macho.
Open recruitment ni sera tu ya serikali katika mambo ya uajili,lakini nani anastahili kupata ajira ni closed selection,nawasihi sana vijana tafuteni taarifa kwa kina,ili mjuwe ukweli,haya mambo yanasikitisha sana.
 
Huo ni ukweli usiopingika,sekretarieti ya ajira imepoteza kabisa dhamira yake kwa sasa,Nina ushahidi wa kutosha jinsi Mashirika na Taasisi za serikali zinavyotoa shinikizo kwa chombo hiki juu ya wakina nani wanatakiwa waajiliwe.Mfano usaili uliofanyika hivi karibuni wa Tanroads.

Fafanua zaidi usahili wa Tanroads ulikua na nini?
 
Funguka mkuu..usaili wa Tanroads ulikuwa na walakini?
Ni vizuri wadau waweke wazi haya mambo ili wanaotafuta kazi wajue...sio unajitutumia unaenda kwa interview ya kazi ambayo imeshapewa mtu tayari..thats unfair!!
 
Mkuu khetewesa ndo kwa mara ya kwanza mm nakusikia kwamba umeapply utumish haujaitwa mm najua siku zote utumish ukiapply na una vigezo vyote hasa original certificate zote lazima uitwe mkuu ,labda kama upo kwenye taasisi ya serikali kwa mkataba na haupitishi barua kwa mwajili kama wanavyotaka mbali na hapo labda utusaidie ni kozi gani ulisoma labda wadau watatoa msaada wa kina
 
Fafanua zaidi usahili wa Tanroads ulikua na nini?

Watu wapo tayari wanasubiri barua za kuitwa kazini tu.Hawa jamaa ni hatari sana jaribu kuangalia hata michakato yao ya ajira katika mizani.Unakumbuka kuna kipindi mwakyembe alitengua ajira za baadhi ya waajiliwa katika mizani?
 
Funguka mkuu..usaili wa Tanroads ulikuwa na walakini?
Ni vizuri wadau waweke wazi haya mambo ili wanaotafuta kazi wajue...sio unajitutumia unaenda kwa interview ya kazi ambayo imeshapewa mtu tayari..thats unfair!!

Kuna watu tayari kwa hizo nafasi,Sekretarieti wanaamlishwa tu.
 
Back
Top Bottom