kaka sijui unapinga nini? Nilijibu hoja lako
"Kwani Kutunza mifupa ni kazi??!!.. kumbuka hiyo mifupa ilikuwa fossilized for thousands of years underground with natural preservative treatment, .. if at all any preservative treatment is required to keep it.. part of the money (tourism fees) collected would be used".
Hapa nasema 1) Ndiyo kutunza mifupa ya kale ni kazi kubwa na ghali, 2) tusiwaze maonyesho yake yataleta faida ya kifedha kutokana na kiingilio maana gharama za kutunza ni kubwa kuliko kila kila kiingilio..
Kwa hiyo anayetaka kuirudisha mifupa aseme jinsi atakavyolipa gharama (Kwanza kujenga ukumbi, pamoja na tekinolojia ya AC, usalama na taa, pili kufunza wataalamu wa fani husika, tatu kugharamia uendeshaji endelevu wa makumbusho mapya.)
Nigeria wanapanga sasa kuchukua hizo sanamu ndogo za bronzi zilizoibiwa na Waingereza mjini Benin. Kwa kazi hiyo wametenga mamilioni kujenga makumbusho mapya. Wakiamua kutumia milioni kutoka pesa ya mafuta yao, sawa,
(hata kama bado watu wengi sana pale wako maskini na bila huduma - chanzo cha BokoHaram). Na Ujerumani waliamua kuwapa bronzi kutoka Benini zilizonunuliwa na makumbusho ya Ujerumani.
Kwa hiyo sidhani Wajerumani watagoma kurudisha mifupa ya dinosauri. Ila ukiangalia maelezo ya ile kamati ya bunge (video), hawasemi wanataka mifupa, wanasema wanataka asilimia ya mapato.
View attachment 1769752
Ambayo naona ni ajabu kidogo ukitaka sehemu ya mapato ya biashara inayoleta hasara. Hao wa pale kama ni wajanja wangejibu je mnataka 50% za hasara ya maonyesho?
Hawatasema, lakini je ingekuwa busara kurudisha mifupa hapa TZ sasa, wakati hakuna mahali pa kuwekea, hakuna wataalamu wanaoweza kuiunganisha na kusimamisha na hakuna pesa ya kuendesha?
Mifupa hii itendewe kama mwendokasi?