Mapato ya Madini yazidi kupaa

Mapato ya Madini yazidi kupaa

mamayoyo1

JF-Expert Member
Joined
Jul 25, 2018
Posts
1,011
Reaction score
1,019

Serikali imesema mapato ya Wizara ya Madini yameongezeka kutoka Sh. bilioni 196 mwaka 2016 hadi Bilioni 310 mwaka 2018/19.

Kuongezeka kwa mapato hayo, kunatajwa kuchangiwa na marekebisho ya Sheria ya Madini ya mwaka 2010 yaliyofanywa mwaka juzi na kuanzishwa kwa masoko ya madini.

Hayo yalisemwa na Waziri wa Madini, Dotto Biteko, alipokuwa akizindua soko la kimataifa la madini jijini Arusha.

Alisema mwaka 2018, baada ya marekebisho ya sheria, mapato hayo yalifikia Sh. Bilioni 265.

“Serikali imekuwa ikichukua hatua mbalimbali kwa ajili ya kuongeza manufaa ya sekta ya madini kwenye uchumi mkubwa wa nchi, sekta hii imefanyiwa marekebisho mbalimbali ili mchango wa sekta hiyo uzidi kuongezeka."

Alisema awali kabla ya marekebisho hayo mchango wa sekta ya madini katika uchumi wa taifa ulikuwa mdogo ukilinganishwa na sekta nyingine na kuwa baada ya mabadiliko ya sheria mchango umeanza kukua na kuongezeka.

“Baada ya marekebisho ya sheria mchango wa sekta ya madini umetoka asilimia 3.5 hadi kufikia asilimia 5.07 mwaka 2018 na tunakusudia ikifika mwaka 2025 ufike asilimia 10, na tutafikia kwa sababu hakuna kipindi nasimama nikiwa na furaha nikikutana na wachimbaji kama sasa hivi, wanalipa kodi vizuri."

“Mapato ya juu tuliyowahi kuwa nayo kwenye madini kabla ya marekebisho ya sheria ilikuwa Sh milioni 943, mwaka 2016 hali ilikuwa mbaya zaidi mapato ya juu ya Tanzanite ilikuwa Sh milioni 700. Wachimbaji wadogo peke yao wameshachangia zaidi ya Sh bilioni 2.7, yote hii ni kwa sababu wachimbaji wameitikia wito na kukubali kulipa kodi,” alisema.

Kuhusu mapato ya madini ya Tanzanite ambayo yanapatikana Mirerani mkoani Manyara, alisema baada ya kujengwa kwa ukuta katika eneo hilo, yameongezeka kutoka kilo 147.7 mwaka 2017 hadi kufikia kilo 949.
 
Yanatunufaisha vipi Watanzania kama yanaishia kukwapuliwa na mkwapuzi mkuu wa magogoni?

2.4 trillions zimepotelea wapi!?

#mamayoyo1 unaandikia gazeti gani, coz leo umekuja na habari za ufuta na madini tu...😀
 
ni habari njema sana,sasa viongozi wetu watapata posho na marupurupu vizuri bila usumbufu..
 
Mapato juu ila unafuu wa maisha hatuuoni Dotto...
Mnakwama wapi kumwambia ukweli mdingi?
 
ni habari njema sana,sasa viongozi wetu watapata posho na marupurupu vizuri bila usumbufu..

Na ndipo Mapato yanapo potelea Mkuu ,wakiona Mfuko umenona hawakawii kuanzisha Mikoa mipya na blah blah za hapa na pale ,hawawafikirii wenye uhitaji zaidi yao ila wanafikiria kutumbua tu.
 
Fursa kama hizi zinatakiwa ziendelee kubuniwa shida ya watendaje wetu wanasubiri mpaka Mheshimiwa Rais ndiye aseme wanamzeesha bure kwa kufikiria sana.
 
Back
Top Bottom