Mapato ya fine za Trafiki zikasaidie kujenga alama na mataa ya barabarani

maharage ya nazi

JF-Expert Member
Feb 7, 2012
344
230
Habari wanaforum. Napendekeza mapato ya fine za polisi usalama wa barabarani za mamilioni na mabilioni zikasaidie kujenga na kurekebisha miundo mbinu za barabarani kama alama na taa za watembeaji kwa miguu na wakatishaji barabara, taa za kuongozea gari, alama za barabarani, njia za zege kwa watembeaji kwa miguu n.k. hii nafkiri itakuwa ni njia sahihi ya kuboresha usalama wa barabarani. Changia katika hili
 
Mtoa hoja amejiweka katika kundi la watanzania wanaoipenda nchi yetu! Imekuwa ni jambo la kawaida kumsikia afande Sirro akitaja mapato lakini sijamsikia akitaja matumizi! Hapa panakuwa sio sawa! Fikiria mapato haya kandamizi kwa dsm pekee kwa siku nane pekee yanafikia million 600! 0.6 bilion je? kwa mwexi wote January itakuwa shilling ngapi? Kwa hesabu za haraka ni zaidi ya billion mbili! Sasa mbona matumizi yake yamekuwa siri kuu!
Kuna mengi yanaweza kufanywa ni hii michango ya tozo, moja likiwa na uboreshaji wa alama za usalama barabarani! Fikiria unakuta kibao cha speed limit kimezibwa na miti au hata kimegongwa na kuanguka chini hakionekani na unalazimishwa kwa nini hukuheshimu alama! Ninapendekeza hivi vibao ili kuleta attention viwekwe juu ya barabara across! Vikiwa na ishara nyingi kuashiria hatari! Jingine la muhimu ni kwa ndugu zangu askari kushauriana na wajenzi tanroads kuhusu umuhimu wa kuweka njia za waenda kwa miguu! Ni jambo la aibu sana unakuta manispaa au tanroads wanajenga barabara na hawafikirii kuweka njia ya waenda kwa miguu! Hii ni hatari sana Fikiria hizi barabara unakuta recently zimejengwa na hawa tanroads hawaoni umuhimu wa kuweka pedestrian way! Mifano ipo mingi kama barabara xote za manispaa, barabara nyingi za tanroads, mifano ni external kisukuru, Goba, mwenge morocco, mifano ipo mingi na zote haziakisi ukuaji endelevu wa jiji! Njia za waenda kwa miguu ni muhimu tanroads mnatakiwa mjiongeze! Mnapokwenda Japan study tour mnafikiri ni kupiga selfie tuu?
 
Kufagiliwa tu inashindikana sembuse kuwekwa mataa? barabara nyingi huku Temeke zimejaa michanga mpaka unashindwa kutambua hii ni ya lami au ya mchanga! akili yao kupunguza ajali ni kupiga faini za mwendokasi tu swala la miundombinu wao hawalijuwi.
 
Bado tupo kwenye ununuzi wa ndege,hela ya miundo mbinu tumetenga fungu kutoka kwenye pesa za rambirambi
"muniombee"
 
Mtoa maada unaakiri sana. Kilomita moja ya barabara ni bilion 1 tu!! Kwa mabilioni hayo yaliyokusanywa so far yangeenda kutengeneza barabara mbadara leo akachube, st maries na nyingine nyingii zingekuwa mkeka!
 
Nadhani kwa jambo kama hilo Serikali itakuwa imefanya la maana.
 
Wanatia mfuko upi serikali ? Mbona sio chanzo cha mapato kwenye bajeti? Wanapswa kutolea maelezo sana CAG tueleza. Wazo safi sana
 
Umeongea point, alama za barabarani zimepinda hovyo hovyo, mataa ya barabarani yananing'inia, machafu, yameoza, hayana solar power backup..., zebra zimefutika, nobody cares!
 
Mtoa hoja amejiweka katika kundi la watanzania wanaoipenda nchi yetu! Imekuwa ni jambo la kawaida kumsikia afande Sirro akitaja mapato lakini sijamsikia akitaja matumizi! Hapa panakuwa sio sawa! Fikiria mapato haya kandamizi kwa dsm pekee kwa siku nane pekee yanafikia million 600! 0.6 bilion je? kwa mwexi wote January itakuwa shilling ngapi? Kwa hesabu za haraka ni zaidi ya billion mbili! Sasa mbona matumizi yake yamekuwa siri kuu!
Kuna mengi yanaweza kufanywa ni hii michango ya tozo, moja likiwa na uboreshaji wa alama za usalama barabarani! Fikiria unakuta kibao cha speed limit kimezibwa na miti au hata kimegongwa na kuanguka chini hakionekani na unalazimishwa kwa nini hukuheshimu alama! Ninapendekeza hivi vibao ili kuleta attention viwekwe juu ya barabara across! Vikiwa na ishara nyingi kuashiria hatari! Jingine la muhimu ni kwa ndugu zangu askari kushauriana na wajenzi tanroads kuhusu umuhimu wa kuweka njia za waenda kwa miguu! Ni jambo la aibu sana unakuta manispaa au tanroads wanajenga barabara na hawafikirii kuweka njia ya waenda kwa miguu! Hii ni hatari sana Fikiria hizi barabara unakuta recently zimejengwa na hawa tanroads hawaoni umuhimu wa kuweka pedestrian way! Mifano ipo mingi kama barabara xote za manispaa, barabara nyingi za tanroads, mifano ni external kisukuru, Goba, mwenge morocco, mifano ipo mingi na zote haziakisi ukuaji endelevu wa jiji! Njia za waenda kwa miguu ni muhimu tanroads mnatakiwa mjiongeze! Mnapokwenda Japan study tour mnafikiri ni kupiga selfie tuu?
Nakubaliana na nyinyi na kama hii hoja inaonekana ni kitu muhimu basi wanaforum waipiganie kwa kuchangia kwa sana na kuipigia kura sana ili wahusika wapate message akiwemo waziri wa ndani na waziri wa ujenzi. Fine haziwezi kulipwa kufaidisha watu huku barabara zetu na miundo mbinu zake zikawa dhoofu. Hatulipi fine kuneemesha polisi. Polisi wanalipwa na serikali.
 
Kwanza tujue polisi wanakusanya tu na hawaruhusiwi kutumia walichokusanya.
Pia tanroad ndo tuwashauri watengeneze barabara bila kutaja chanzo cha mapato kwan pesa zote huenda basket fund huko hazina.
Niko tayari kukosolewa
 
Back
Top Bottom