Petro E. Mselewa
JF-Expert Member
- Dec 27, 2012
- 10,346
- 26,138
Asitokee mtu kujifanya yeye hafanyi. Isisikike sauti ya kulaumu kinachoendelea kwakuwa wote wanafanya sawa. UKAWA dhidi ya CCM na washirika wake wanaendelea na mapambano ndani na nje ya Bunge la Katiba. Mapambano ya kujenga na kuimarisha demokrasia na mustakabali wa Taifa hili.
UKAWA wameanza mikutano ya nje ya Bunge.Wameanzia Mwanza. CCM nao,kwa mwamvuli wa ziara za Katibu Mkuu wao Kinana,wanatembea wakijadili masuala hayo hayo ya Katiba kwenye mikutano ya hadhara. Walianzia Mwembeyanga Temeke,jijini Dar es Salaam. Mwigulu Nchemba,Naibu Katibu Mkuu wa CCM-Bara,ameibukia kanisani na kueleza kuhusu Katiba mpya.
Nasema asije akaonekana mmoja ni mkorofi na mwenye kuharibu mchakato wa Katiba mpya.Kwakuwa pande zote ziko kwenye mapambano. Na kwenye mapambano,mbinu mbalimbali hutumika. Asiombe mtu poo. Katiba ni Sheria mama ya nchi.Kuandikwa kwake lazima kuambatane na mapambano ili ikipatikana ipatikane yenye meno kweli. Katiba nzuri haitapatikana kwa lelemama.
UKAWA pigeni kazi nje na ndani ya Bunge;CCM endeleeni kukisemea na kukisimamia mnachokiamini. Mapambano yanaendelea..