Mapambano ya Amani Kupinga Tozo Dhulumati za Miamala

Bams

JF-Expert Member
Joined
Oct 19, 2010
Posts
19,768
Reaction score
49,934
Wananchi hatupingi kuchangia shughuli za maendeleo kwaajili ya ustawi wa Taifa letu, lakini uchangiaji huo uwe unazingatia uhalisia wa maisha ya watanzania.

Wananchi tutambue kuwa hatuna wa kututetea. Serikali inatudidimiza badala ya kutuwezesha. Bunge linatuzika badala ya kutufufua.

Tukisema tuandamane ili kuelezea hisia zetu za kutoridhishwa na ongezeko la zaidi ya 100% kwenye huduma za utumaji na upokeaji fedha kwa kupitia mitandao ya simu, mjue akina afande Muroto bado wapo hai, wao wanajua kuwa kazi kubwa ya Polisi ni kutoa kipigo cha mbwa koko na siyo kuwalinda raia.

Chaguo tulilo nalo ni hili ambalo hakuna atakayetugusa:

1) Wananchi tujibane kwa namna yoyote tuwezayo, kila mmoja asitume wala kutoa fedha kupitia mtandao wa simu kwa muda wa siku 14. Hiyo iwe ni kuanzia leo.

2) Wananchi tusitumie simu za mkononi kuongea kwa siku 14, isipokuwa kwa dharula tu kama vile ugonjwa na misiba. Mawasiliano yawe kwa sms, fb na whatsapp.

3) Kila mmoja ajitahidi kuwapata watu wasiopungua 20 ambao nao watafikishiwa ujumbe huu, na wao wawafikishie wengine.

Ukombozi wetu upo mikononi mwetu wenyewe. Mtambue ukombozi una gharama kubwa. Wapo waliopoteza maisha, ndiyo sisi tukawa huru. Wapo waliofungwa ndiyo sisi tukawa huru. Wapo waliolemazwa, ndiyo sisi tukawa huru. Sisi, hakuna atakayekufa, hakuna atakayepata ulemavu, hakuna atakayefungwa kwa kujitoa katika hili. Maumivu yatakuwepo kiasi kidogo sana kwa kuikosa huduma tuliyokuwa tumeizoea

Wanaounga mkono wagonge like. Na tusiishie kwenye kubonyeza like. Ukigonga tu kitufe cha like, toka dakika hiyo unaanza kutekeleza.

Maoni ya namna ya kuboresha litakuwa ni jambo jema.
 
Hii nchi ina ujinga mwingi sana, na ujinga ndio rafiki mkuu wa watawala.
 
Mkuu ushauri huu unawapa hawa watanzania wasiojielewa? Hawa ambao ni nusu wafu?
 
Wabongo wana umoja kwenye maswala ya kipuuzi tu 😂 kuchamba kama alivyosema yule kiongozi flani!

Vitu vya msingi ni kama kumpigia mbuzi gitaa tu
 
Tupaze sauti Bila kuogopa,tena tupaze sauti mpaka nchi wahisani tuwaeleze jinsi tunavyoibiwa.
Kina Zito,Maria,fatuma karume naona bado wanaendelea kunutrilize Ili kuonekana kweli Walikua wapinzani.
Watoto wa wanyonge ni sisi tu na si FATUMA KARUME ALIYEZALIWA NA KUMALIZA P YAKE IKULU,SI FATUMA ALIYELELEWA NA KULA MIPENSHENI YA IKULU.

WOTE TUUNGANE KUPIGANA HII VITA
 
Huwajui watanzania wewe

Vipi ongezeko la la shilingi 100 kwenye Bei ya mafuta ?

Vipi Ongezeko la Bei zA vifurushi ?

Watanzania ni maiti zinazotembea utapoteza muda wako bure kuoambania maiti haki zao. Jikwamue wewe na familia yako mkuu.
 
Bora ya mama kuliko yule tapeli aliyekuwa anakwapua pesa zetu na kwenda kujijengea uwanja wa ndege kijijini kwao
Sasa hizi za sasa ndio utacheka na land cruiser mpya imetoka juzi 😅😅😅hakuna cha madarasa wala barabara!

Naskia Mzee wa Tozo ya Mshikamano ameingiza moja tayari!
 
🤣👇
android-NnFb.png
 
Huwajui watanzania wewe

Vipi ongezeko la la shilingi 100 kwenye Bei ya mafuta ?

Vipi Ongezeko la Bei zA vifurushi ?

Watanzania ni maiti zinazotembea utapoteza muda wako bure kuoambania maiti haki zao. Jikwamue wewe na familia yako mkuu.
Fact.
 
Kwenye hili, bodaboda wajipange vizuri. Watafanya biashara ya uhakika.

Nimeanza kutekeleza azma yangu. Kuna mtu ilikuwa anitumie hela sh 800,000. Kwa kawaida huwa anatuma kwa Mpesa. Nimemwambia sitaki atumie hiyo njia. Akanihakikishia kuna bodaboda huwa anamtumia, mwenye uaminifu mkubwa. Ameniletea, nikamwuliza gharama amesema sh 4,000. Nikaamua kumlipa sh 10,000. Nimemwusia, azingatie sana uaminifu, atakuwa na nafasi nzuri zaidi kufanya hii kazi ambayo unatembea bila mzigo.
 
Back
Top Bottom