mwengeso
JF-Expert Member
- Nov 27, 2014
- 9,286
- 6,727
Kichwa cha mada hii ni cha gazeti la Mwananchi - alhamisi, septemba 10, 2015 kuhusu makala ya Prof. L. Lipumba.
Kabla ya kuchangia makala hiyo niwaombe wana jamvi tupunguze kuweka picha za nyomi za mikutano ya kampeni kana kwamba ndiyo kura halisi. Tuchukue muda wetu kurejea sera, ilani za vyama na ahadi za wagombea kwenye kampeni kama zinakidhi matarajio yetu ya mabadiliko. Mimi ninayaita mabadiliko ya kifikra na kiutendaji kwa kila Mtanzania. Hivyo kura yangu nitampa kiongozi yule tu atakaye nishawishi kuwa anayo mikakati ya kuleta mabadiliko hayo.
Prof. Lipumba kwenye makala hiyo anasema: "Rushwa na ufisadi ni adui wa haki na pia ni kikwazo kikubwa cha maendeleo.... Madhara ya rushwa ni mengi. Viongozi wanatumia vibaya madaraka yao kwa maslahi binafsi. Inasababisha Serikali na Asasi zake kushindwa kufikia malengo yake. Mapato ya Serikali hayakusanywi ipasavyo". Anatoa mfano wa Rwanda ambako imeundwa Ofisi ya Mchunguzi Maalum (Ombudsman) inayosimamia na kuratibu kuzuia na kupambana na rushwa, kwetu ni TAKUKURU. Pia Rwanda imeanzisha "Baraza la Ushauri la Taifa la kuzuia na Kupambana na Rushwa. Pia kuna Mabaraza ya Ushauri katika ngazi za chini." Amenukuliwa Prof. Lipumba.
Kwenye kampeni zinazoendelea tumemsikia JPMagufuri akiahidi kuunda mahakama ya kushughulikia mafisadi na kwamba akiingia tu madarakani ni kuwakamata hao mafisadi. Kwa jinsi anavyotamuka ni wazi hilo linatoka moyoni mwako na kwamba anatambua na kubainisha 'rushwa na ufisadi' ni kero namba moja ya watanzania na maendeleo. Gazeti hilohilo la Mwananchi, limenukua kampeni zake Mkoani Tanga kwamba "Dk Magufuri alisema anataka Serikali yake iwe rafiki kwa wafanya biashara wote, lakini wawekezaji wakubwa ni lazima waondolewe misamaha ya kodi isiyokuwa na tija ili fedha zitakazopatikana zisaidie kuendeleza miradi mbalimbali ya Serikali". Hilo likiwa jibu la Prof Lipumba kuhusu mapato ya Serikali kutokukusanywa ipasavyo kwa sababu ya kukithiri kwa vitendo vya rushwa.
Nahitimisha kwa kusema hadi sasa ni mgombea Urais wa CCM (Dk Magufuri), tofauti na vyama vingine, ambaye amejipambanua wazi kwamba rushwa na ufisadi ndio adui na moja wa maendeleo ya nchi hii. Nitampa kura yangu.