Mapacha wafa maji, mama ajitupa baharini siku ya Eid

Mapacha wafa maji, mama ajitupa baharini siku ya Eid

Donatila

JF-Expert Member
Joined
Oct 23, 2014
Posts
8,247
Reaction score
25,191
Kamanda wa Polisi mkoa wa Kagera, Agustino Ollomi alithibitisha kutokea kwa tukio hilo.

Kamanda Ulomi alisema juzi majira ya saa 11:30 jioni, mapacha hao walikuwa wakiogelea ziwani katika eneo la Kiloyela lililopo katika Manispaa ya Bukoba mkoani humo.

Marehemu mapacha hao walitajwa kuwa ni Hussein Hamis (12) na Hassan Hamis(12), na kwamba walikuwa wanafunzi wa darasa la saba katika Shule ya Msingi Kashai.

“Watoto hao walikuwa wa askari mwenzetu(wa) kitengo cha Usalama Barabarani," alisema Kamanda Ollomi na kwamba "walikuwa wakisoma darasa la saba.”

Alisema sababu ya kifo cha marehemu hao ni kuzidiwa na nguvu ya maji na kupelekea kuzama ambapo waliopolewa wakiwa wamefariki.

"Watoto wenzao baada ya kuona wenzao wakiendelea kuzama walipiga kelele ili kuomba msaada, lakini jitihada za kuwaokoa wakiwa hai zilishindikana," alisema.

"Tayari watoto hawa wamezikwa Juni 27 mwaka huu (jana) katika makaburi ya Kishenge, yaliyoko katika Manispaa ya Bukoba.

“Tunaendelea kuwasihi wazazi, kuendelea kuangalia usalama wa watoto wao hasa katika siku za sikukuu ili kuepusha madhara kama haya."

Jijini Dar es Salaam, mwanamke aitwaye Asha Yahya(30), mkazi wa Zanzibar anadaiwa kujirusha baharini akiwa katika kivuko cha MV Magogoni kwa lengo la kujiua, lakini wananchi waliwahi kumuokoa.

Kamanda wa Polisi mkoa wa Kipolisi Temeke, Andrew Satta alisema tukio hilo lilitokea majira ya 2:10 asubuhi wakati akitokea Kigamboni kuelekea Ilala na kwamba sababu za kutaka kujiua ni wivu wa kimapenzi.

"Baada ya kumhoji alituambia kwamba sababu ya kutaka kujiua, eti mume wake anataka kuoa mwanamke mwingine," alisema Satta.

Katika tukio jingine katika kipindi cha sikukuu, Jeshi la Polisi jana liliokota mwili wa mtumishi wa Mamlaka ya Bandari (TPA), Masoud Abdulrahman(27) katika ufukwe wa Kisiwa cha Mbutu, kilichopo Kigamboni.


Kamanda Satta alisema marehemu kabla ya kukutwa na umauti huo alikuwa na wafanyakazi wenzake 20 ambao walikwenda katika ufukwe huo kwa ajili ya kufurahia sikukuu ya Eid, lakini wakati wakiogelea wimbi kubwa la maji liliwapiga na hivyo wote kupotea.

Alisema hata hivyo, baada ya Jeshi la Polisi kufanya msako baada ya kugundua kwamba kuna watu waliosombwa na maji, waliwapata wenzake 20 ambao waliokolewa na kukimbizwa hospitali.

Kwa upande wa mkoa wa kipolisi wa Ilala, mtu mmoja ambaye jina lake halikujulikana mara moja aligongwa na basi la mwendokasi katika Barabara ya Uhuru na kufariki papohapo juzi pia.

Kamanda wa Polisi wa Ilala, Salum Hamdani, alisema mtu huyo aligongwa na gari hilo baada ya kuingilia barabara ya mwendokasi na kwamba mwili wa marehemu umehifadhiwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili.


Chanzo: Nipashe
 
Siku kama hizi huwa na matukio yake.Ni muhimu sana kuchukua tahadhari hasa kwa watoto.Wapumzike kwa amani
 
Kichwa cha habari kinachanganya sana. Unaweza kudhania habari tofauti kabisa.

Binafsi nilidhani hao mapacha wamekufa wakiwa wanamfuata mama yao aliyejutupa baharini,dah!
 
Inasikitisha mno tunapopeteza watanzania wenzetu katika mazingira kama haya,poleni wafiwa wote na Mwenyezi Mungu awapeni wepesi;FUNZO HAPA,jeshi letu la polisi liimarishe patrol zake hasa kwenye mikusanyiko ya watu wakati wa sikukuu kama hizi,yaanzishwe mafunzo maalum kwa coast guards ambao wasambazwe kwenye fukwe zetu kwa ajili ya usalama,kazi zao ziwe ni kutoa msaada wa kwanza kwenye dharura kama hizi,wao pia wawe na uwezo wa kuruhusu eneo gani litumike kwa uogeleaji na hili linafanikiwa kwa kutumia bendera zenye rangi tofauti kutegemeana na hali ya ufukwe,na watu waruhusiwe kuogelea penye uwepo wa coast guards only,pia wawepo shark spotters kwa ajili ya kuonya watu kama sharks wapo karibu na watu;lengo ni kujifunza ili tukio lisitokee tena.
 
Haya magari ya mwendo kasi yawe yanaangalia hata kama mtu havuki kwenye zebra sio kusababisha ajali za lazima wenye ni kutak sifa tu
siku moja gerezan tunavuka kwenye zebra anatak aiingie kituon akalikunja moja kwa moja bila kuangalia mbele kuna watu wanavuka tena kwenye zebra ikabidi tukimbie tu
 
Back
Top Bottom