Maonyesho ya kimataifa ya biashara ya huduma yamalizika

Maonyesho ya kimataifa ya biashara ya huduma yamalizika

Yoyo Zhou

JF-Expert Member
Joined
Jun 16, 2020
Posts
200
Reaction score
323
Maonyesho ya Kimataifa ya Biashara ya Huduma ya China kwa mwaka 2020 yamefanyika mjini Beijing kuanzia tarehe 4 hadi 9 Septemba yakiwa na kaulimbiu ya "Kutoa Huduma Duniani, Kuleta Faida ya Kunufaishana." Kampuni 18,000 kutoka nchi na sehemu 148 duniani zinashiriki katika maonyesho haya makubwa ya kwanza ya kimataifa kufanyika mwaka huu tangu mlipuko wa virusi vya Corona kutokea.

Akihutubia mkutano wa viongozi wa maonyesho hayo Ijumaa iliyopita kwa njia ya video, Rais Xi Jinping wa China ametoa mapendekezo matatu kuhusu ushirikiano wa kufungua mlango katika sekta ya utoaji wa huduma. Mapendekezo hayo ni kujenga kwa pamoja mazingira shirikishi na kufungua mlango wa kufanya ushirikiano, kuchochea kwa pamoja msukumo wa ushirikiano unaongozwa na uvumbuzi, na kuweka mazingira ya ushirikiano ya kunufaishana na kupata faida kwa pamoja.

Maonesho hayo si kama tu yameonesha nia thabiti ya serikali ya China katika kukabiliana na matatizo kwa sasa na changamoto katika siku za baadaye, bali pia yameonesha moyo wa dhati wa China kufungua mlango na kuzingatia ushirikiano wa kimataifa.
Kivutio kikubwa katika maonyesho hayo imekuwa ni roboti za aina mbalimbali zinazofanya kazi tofauti ikiwemo kuua vijidudu, kusambaza vifurushi.

Mkurugenzi wa Usanifu kwenye Kampuni ya Uvumbuzi na Teknolojia ya Candela (Shenzhen) inayotengeneza roboti za Candle By.Zhang Wenyi amesema, roboti zilizotengenezwa na kampuni hiyo zilifanya kazi usiku na mchana wakati wa mlipuko wa virusi vya Corona. Amesema kampuni yake ilipeleka roboti kadhaa katika hospitali za muda za Huoshenshan, Leishenshan na Jinyintan ili kusaidia katika mapambano dhidi ya virusi vya Corona katika mji wa Wuhan katika siku za mwanzo za mlipuko wa virusi vya Corona.

Nchi mbalimbali za Afrika zilishiriki katika Maonyesho ya Kimataifa ya Biashara ya Huduma yaliyofanyika hapa Beijing. Kama inavyofahamika, Afrika ni bara linalotambulika sana kutokana na kuwa na rasilimali kubwa ya vivutio vingi vya utalii. Pamoja na kuwa sekta hiyo imeathirika vibaya na janga la virusi vya Corona, nchi za Afrika zilitumia fursa ya Maonesho hayo kuwavutia watalii wengi zaidi wa China kutembelea vivutio vinavyopatikana katika nchi hizo.

Pia Jukwaa la 5 la Siku ya Afrika kwenye Maonesho ya kimataifa ya biashara ya huduma lililoandaliwa na Baraza la viwanda kati ya China na Afrika (CAIF) lilifanyika jumatatu kwenye Kituo cha Mikutano ya Kimataifa hapa Beijing, likiwa na kauli mbinu ya "Kipindi Baada ya COVID-19 na Fursa Mpya kwa Afrika".

Akihutubia katika jukwaa hilo, Katibu mkuu wa Baraza la CAIF Bw. Cheng Zhigang amesema kuwa chini ya hali mpya ambayo uwekezaji na ugavi kutoka kwa nchi za magharibi vinapungua na janga la COVID-19 linaendelea, kuhimiza ushirikiano kati ya kusini na kusini kutazisaidia nchi za Afrika kupunguza athari za janga hilo, na pia ni chanzo kipya cha uwekezaji katika mchakato wa kuendeleza viwanda barani Afrika.
 
Back
Top Bottom