MAONO YA JANGWANI.

MAONO YA JANGWANI.

Dotto C. Rangimoto

JF-Expert Member
Joined
Nov 22, 2012
Posts
1,985
Reaction score
1,286
ange angel.jpg



MAONO YA JANGWANI.
1.
Kwa macho haya mawili,
Nilishuhudia,
Vinginevyo yapofuke.
2.
Kwa masikio mawili,
Niliyasikia,
Kinyumeche yazibike.
3.
Malaika elfu mbili,
Menisimamia,
Kwa vishindo na makeke.
4.
Nikapelekwa mahali,
Ninawaapia,
Sipajui jina lake.
5.
Nikitetemeka mwili,
Ninawahofia,
Nusu mkojo utoke.
6.
Mmoja mwenye kauli,
Kanikaribia,
Kakunja magoti yake
7.
Siogope rijali,
Akaniambia,
Asemayo niandike.
8.
Makaratasi na stuli,
Akanipatia,
Ujiti na wino wake.
9.
Kwa nahau na methali,
Akasimulia,
Dunia na mwendo wake.
10.
Simba ataka kimwali,
Akamchumbia,
Dondoro akawa mke.
11.
Fisi kapewa shughuli,
Yakustajabia,
Supu ya nyama apike.
12.
Kanu kapawa kibali,
Kuwahudumia,
Kuku wasihadhirike.
13.
Dhalimu avishwa shali,
Kuwapigania,
Madhulumu wakomboke
14.
Haramu sasa halali,
Mnaangamia,
Mlipo sasa mtoke.
15.
Yote haya yana dali,
Asema Jalia
Na mtake msitake
16.
Mfanye kwa kulla hali,
Tunawausia,
Njia ya Mola mshike.
17.
Muisimamie kweli,
Haki iwe njia,
Kama mwataka mfike,
18.
Simpendelee dhuli,
Ila pigania
Apewe kilicho chake.
19.
Shirki na iwe mbali,
Kiikaribia,
Mtakosa radhi yake.
20.
Majazi na taawili,
Hutayakimbia,
Hivyo mjuzi msake.
21.
Tulosema si kalili,
Kikomo twatia
Tunataka mzinduke.

29/10/2016

Kwa kazi zangu nyingi za ushairi, naomba like page yangu ya facebook kwa kubofya link hiyo.

Mashairi Ya Rangimoto | Facebook

Dotto Rangimoto Chamchua(Njano5)
Call/Whats app 0622845394 Morogoro.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom