Juzi Jumamosi Kuamkia Jumapili niliota Ndoto ya Maono ya Ajabu sana, sana
Kuna Mwanasiasa ambaye wa aina yake Alikula nyasi, lakini huyu yeye Mungu atamnyanyua Fasta Fasta! Sababu hasa ikiwa Kutumia Ushirikina huku akimtaja Mungu, Kumchanganya Mungu na Matunguri na Kutoa Makafara!
Simsemi Mtu ila Kama anajijua Ananafasi ndogo Kama Ukucha Kutubu! Heeeee Mbona Itakuwa Taharuki? Niliona sikia Ngurumo kubwa sana, sana, ya radi iliyoambatana na Maneno makali yakitokea angani, Sauti yake Utadhani ni ya Maspika Makubwa 1000! Kisha ile sauti Ikaisha, Nikamwona Mtumsimtaji, Akiwa amesimama amezungukwa nanwapambe! Ni ajabu hakusikia Makelele yote yale! Nilishangaa! Mawingu yakaanza kutanda, Watu wakaanza Kuondoka, Akapaza sauti, "Msiondokeee hii mvua itapitaa, Jamani msiondokee hii mvua Itapitaaa!"
Ghafla Mvua Kubwa sana Ikashuka Angani, Matone yake yalikuwa kama maji Machafu! Ilipofikia
Kimo
cha Mabega yake, yale matone ya mvua yakafanya U turn kama Parabola, Yakamchota na Kupaa naye angani huku yakimviringa Viringa. Hakuna hata tone moja liligusa ardhi.
Ilikuwa Taharuki! Giza likatanda sana Na watu wakakimbia Pande zote kwa hofu!
Nikajiuliza kwanini mvua, kwanini iwe chafu, maji yanakataje kona na Kupanda angani tena! Nikasikia jibu moyoni, Ni mvua ya Machozi, ni Mvua ya Damu! Nikajiuliza How! Kutokea wapi? Na inampeleka wapi?