Maoni yangu kwa wabunge wapya


G

Gm32

Member
Joined
Nov 2, 2010
Messages
34
Likes
0
Points
0
G

Gm32

Member
Joined Nov 2, 2010
34 0 0
:israel::israel:Habari za Alasiri wanaJF.

Nimefurahishwa na ninaendelea kufurahishwa na matokeo ya upinzani kwa ujumla wake. Sikuzote naamini katika uaminifu na Uwajibikaji, kwa jinsi matokeo yanavyotangazwa kwa upendeleo napata picha kuwa kutawala tanzania kunahitaji mikakati sahihi na yenye kusimamiwa kwa uhakika.

1.Tume ya taifa inahitaji marekebisho makubwa, mwenyekiti na viongozi wa tume wanateuliwa na raisi kwa utashi wake mwenyewe. Hapa lazima Uhuru wa tume utakua na mipaka kiutendaji kwani aliekuteua huwezi kumkatalia jambo atakalo. Tunahitaji viongozi wote wanaoteuliwa wapitishwe bungeni ili wabunge (wawakilishi wa wananchi) waangalie wasifu na kupima utendaji wa wanaoteuliwa.


2. Watanzania ni masikini wa kutupwa, UMASIKINI huu ni mtaji mkubwa kwa viongozi WALAFI NA MAFISADI. kwa sababu moja kubwa:
IN MAKING IMPORTANT DECISIONS POOR ATTACH IMPORTANCE ONLY ON MATTERS RELATED IN ONE NIGHT PLEASURE WITHOUT KNOWING THE ONLY PENALTY OF THAT MISTAKE IS DEATH, ndio maana mtu anauza kura na maisha yake anayaweka rehani kwa miaka mitano kwa sababu tu ya 10,000, kofia na kitenge.


3. Chadema tumepata majiji 3, namshukuru Mungu baadhi ya majimbo tuliyoshinda tuna uwezo wa kuunda serikali za manispaa na za majiji. Chondechonde mliochaguliwa na viongozi wa chadema yatupasa kuonyesha kile tulichotaka kufanya tukiwa chama tawala INCASE TUTASHINDWA KWENDA IKULU THIS TIME. TUFANYE KAZI KWA BIDII. PAMOJA NA KUPAMBANA NA UFISADI LAKINI TUHAKIKISHE UCHUMI NA HUDUMA KATIKA MAJIMBO YETU VINABOREKA HADI AMBAO HAWAKUTUCHAGUA WATAMANI KUHAMIA MAJIMBONI MWETU.


4. Ndio kwanza tuanaanza mapambano HAKIKA CCM HAWATATULIA, watataka kuwakwamisha ili muonekane hamfanyi kazi, pia kuwarubuni madiwani wetu ili wakisaliti chama PLEASE TUWE MAKINI NA TUACHE TAMAA.


5. Tuwahimize wananchi kufanya kazi kwa bidii, wasisubiri neema kutoka mbinguni, tuwawezeshe, tuwatumie wataalamu waliopo, tuwafundishe na kuwapa moyo wananchi jinsi ya kujiajiri kutokana na mazingira yetu tuliyonayo.


6. MAJIMBO TULIYOSHINDA HADI SASA NI MUHIMU SANA KWA UCHUMI WA NCHI YETU BILA KUTEGEMEA SERIKALI KUU, MABARAZA YA MADIWANI WAKISHIRIKIANA NA WABUNGE WAO WAKIWEKA MIKAKATI SAHIHI TUTAINUA UCHUMI WA MAENEO YETU NA TANZANIA KWA UJUMLA NA KUWA VIONGOZI WA MFANO HAPA NCHINI, TUKIJIPANGA VYEMA TUTAWAVUTIA WAPIGA KURA WENGI KUTUCHAGUA KATIKA MAJIMBO MENGINE, TUJITAHIDI KUWASAIDIA WANANCHI KWA MOYO MMOJA.


7. Mheshimiwa Dk Slaa, naomba ukutane na wabunge wapya wa Chadema na wengine wa upinzani, ili uwaelekeze na kuwapa uzoefu wa jinsi ya kupanga hoja bungeni, kuwa na msimamo mmoja wa MSINGI NA MANUFAA KWA TAIFA ZIMA ili kuepuka kuwa vichekesho bungeni na kuwa watu wa kudharaulika mbele ya jamii. Nalisema hili kwa sababu najua kwa sasa ccm itajitahidi kuwaaminisha wananchi kuwa upinzani haufai.


8. Nawaomba kabla ya mbunge wa upinzani kutoa hoja bungeni ni vizuri akaiwasilisha kwa wabunge wenzake ili kuwa na maoni sawa na msimamo mmoja.


9. Nawaomba mkumbuke ya kuwa wananchi wamewaamini KUPITA KIASI, CHONDECHONDE NDUGU ZANGU MSIWAANGUSHE, KUMBUKENI WAPO WALIOTOA MAISHA YAO NA NGUVU ZAO KWA AJILI YA USHINDI HUU, MKIWASALITI HAWA WANANCHI IMANI KWA UPINZANI ITATOWEKA KABISA.Tuwe makini kwenye mienendo na mazungumzo yetu ndani na nje ya bunge, nyie ni kioo cha jamii, kila mtu anataka kuona tofauti yenu na wasindikizaji please TUWE MAKINI, MOYO WA KUWATUMIKIA WATANZANIA.

HAYA NI MAONI YANGU.......

SEE YOU MJENGONI :israel::israel::israel::israel::israel::israel::israel::israel::israel::israel:
 

Forum statistics

Threads 1,252,312
Members 482,076
Posts 29,803,508