Maoni yangu kuhusu uchaguzi UVCCM

Azizi Mussa

JF-Expert Member
May 9, 2012
9,172
7,428
Nimesikia kuwa kuna vijana zaidi ya 100 waliojitokeza kugombea nafasi ya Mwenyekiti wa UVCCM (pekee sijajua kwa nafasi nyingine). Aidha, nimejaribu kupitia pitia majina ya wanaotajwa kugombea na nilichokibaini ni kwamba mengi ya majina ya niliowaona, ni watu ambao sijawahi kuona hoja yoyote ya kisiasa ambayo washawahi kuitoa kokote kwa lengo lolote tangu nimeanza kufuatilia siasa.

Sasa ambacho nimekuwa nikitafakari na pengine kupata mashaka: ijapokuwa kujitokeza kwa wagombea wengi ndio demokrasia, ni kwa nini vijana hawa hawajawahi kutoa hoja yoyote ya kisiasa popote (hadharani)?

Napata mashaka kwamba usije ukakuta tunachokiona ni matokeo ya ukosefu wa ajira "nyomi ya TRA" ambapo kijana huomba kokote anakodhani ni ajira, na hivyo hata watu wasiokuwa na interest na siasa na mambo ya uongozi wanajikuta wakiomba nafasi hizo kama wanavyoomba ajira nyingine. Kama ndivyo, hii ni hatari kubwa.

Ikumbukwe kuwa ili mtu awe kiongozi wa maana ni lazima awe amebeba maono fulani na awe na msukumo wa kuwa "inspire" wengine. Hili ni suala linalostahili kuchukuliwa kwa tahadhari na wahusika ili tuweze kupiga hatua kwenda mbele.

usitembee juu ya ardhi kwa majivuno
 
Jamani, nimetoa angalizo tu na sababu ya angalizo hilo nimetoa vile vile

usitembee juu ya ardhi kwa majivuno
Hivi wewe ni chama gani? Mambo ya ccm unaingilia,mambo ya chadema unaingilia,ACT umo sasa tukueleweje? Ila kumbukumbu zangu zinaniambia u mmoja wa wasaliti waliotimuliwa chadema,almaarufu ' masalia'!
 
Hivi wewe ni chama gani? Mambo ya ccm unaingilia,mambo ya chadema unaingilia,ACT umo sasa tukueleweje? Ila kumbukumbu zangu zinaniambia u mmoja wa wasaliti waliotimuliwa chadema,almaarufu ' masalia'!
Mimi ni chama gani, hilo si muhimu wala halikusaidii kitu.

usitembee juu ya ardhi kwa majivuno
 
Back
Top Bottom