Maoni yangu kuhusu mgomo wa walimu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Maoni yangu kuhusu mgomo wa walimu

Discussion in 'Jukwaa la Elimu (Education Forum)' started by mcubic, Jul 31, 2012.

 1. mcubic

  mcubic JF-Expert Member

  #1
  Jul 31, 2012
  Joined: Mar 3, 2011
  Messages: 10,163
  Likes Received: 4,192
  Trophy Points: 280
  "Elimu ndio ufunguo wa maisha" hii ni kauli maarufu na kila mmoja wetu anafahamu umuhimu wa elimu katika maisha. Elimu kwa maana isiyo rasmi ni mchakato wa kuelimisha ama kuelimishwa jambo usilolijua ili uweze kupata ufahamu chanya ama hasi wa jambo hilo.

  Ni miaka mingi imepita tangu nianze kusikia matatizo ya walimu na serikali, kikubwa walimu wakilalamikia maslahi duni wanayopata huku serikali ikjigamba kutatua matatizo haya pale inapoulizwa.


  Kama nilivyotambulisha awali maana ya elimu kuwa ni kupata ufunuo kwa jambo usilofahamu, hapa wanafunzi wanaelimishwa mambo mbalimbali na walimu katika utaratibu maalum ambao nchi imejipangia ili kuweza kukamilisha malengo mbalimbali.


  Kwa kuwa elimu ni muhimu katika jamii yetu, ubora wa elimu nao ni jambo la msingi katika muktadha wa Nchi yeyote ile. Walimu wanapaswa wapate maslahi bora kuanzia mishahara yao na posho zao ili waweze kutoa elimu bora kwa wanafunzi wao.


  Walimu wanapaswa kuwa na nyenzo bora zitakazowawezesha kutoa elimu bora. Mfano wa nyenzo hizi ni kuwa na vifaa vya kisasa vya kufundishia (ICT), maabara bora, maktaba na wanaoelimishwa kuwa na madawati na vitendea kazi. Haya ni baadhi ya mambo muhimu yanayomzunguka mwalimu na mwanafunzi.


  Endapo mwalimu atakosa mambo haya ya msingi, basi mwalimu huyu kuna uwezekano mkubwa wa kutotoa elimu bora hivyo taifa kukosa wataalamu watakaoliletea tija taifa letu.


  Serikali kwa upande wake inakubali kwamba walimu wanahitaji maslahi bora, wanafunzi pia wanahitaji mazingira bora kiujumla ili waweze kuelimika vizuri, ila tatizo ni uwezo mdogo wa kibajeti. Nijuavyo mimi serikali iliyowekwa madarakani na wananchi inapaswa kutatua kero za wananchi, na si kutoa sababu kwa wananchi ya kutotekeleza ama kutatua kero.


  Serikali ni lazima ihitimishe suala hili kwa kutatua kero za walimu kwa kuangalia chanzo na si matokeo, la sivyo kila mwaka kutakuwa na migongano baina yake na jamii katika kada tofauti. Mgomo wa madaktari una kishindo kikubwa kwa kuwa muathirika huenda akafa, lakini kishindo cha mgomo wa walimu ni kibaya zaidi kwa kuwa muathirika hapati elimu bora, hivyo kushindwa kukabiliana na changamoto za kimaisha.


  Mathalani masomo mengi hufundishwa kwa kuwaandaa wanafunzi kinadharia na si vitendo, hii hupelekea wanafunzi kushindwa katika soko la ajira na pia kupungua kwa ubunifu hapa nchini kwetu.


  Nahitimisha kwa kupendekeza walimu watekelezewe maslahi yao kwa asilimia mia moja, ili watoto wa wakulima waje wapate fursa katika nchi hii, pia mfumo wa elimu ubadilike uwe wakivitendo zaidi ili tupate wabunifu watakaolivusha taifa hili katika janga la umaskini na kuepuka mambo mengi ya kuiga kutoka kwa wanzetu.
   
 2. mgunda1990

  mgunda1990 Member

  #2
  Jul 31, 2012
  Joined: Jul 19, 2012
  Messages: 69
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  huo ndo ukwel..
   
 3. Chiwa

  Chiwa JF-Expert Member

  #3
  Jul 31, 2012
  Joined: Apr 17, 2008
  Messages: 1,348
  Likes Received: 648
  Trophy Points: 280
  binafsi nafikiria vinginevyo kwa kiasi fulani. cha kwanza jamii lazima ielewe thamani na kazi ya mwalimu kwa jamii na ikiwezekana jamii zianze kuchangia kuboresha mazingira mazuri kwa mwalimu ikiwa ni pamoja na kuwapa nyumba allance na ikwezekana kuwapa mazingira mengine ya kipato. mfano shule ipo kijijini ni bora kukatengwa shamba la mwalimu akalimiwa akvuniwa na mwisho wakati wa mauzo hizo gharama zikatolewa naye akabaki na kilichopatikana.
  sio hivyo jamii kwa sasa inajifanya eti kusomesha watoto shule za gharama kubwa ambazo nyingi hakuna cha maana zaidi ya kingereza na bwebwe za kula wali mchana na kubebwa kwa magari kwanini wazazi wasijipange kuboresha shule za mazingira yao na hasa kuwapa waalimu kipato cha ziada
  mwisho waalimu inafika muda lazima wajipange kujiari na sio kutegemea serikali kuwa mwajiri mkuu. hii inawezekana kwa waalimu kutengeneza partnaship za waalimu wasiozidi ishirini na wakaanzisha shule.
  ujenzi wa darasa moja ukisimamiwa vizuri inaweza kuwa kama 12m pamoja na madawati ikawa kama 15m kwa wanafunzi 40 wenye kulipa ada pamoja na michango mingine 600,000 kwa kila mwanafunzi. nadhani nisiendelee na hesabu kwani wao ni waalimu wanaua zaidi yangu.
  hata hivyo poleni sana ila napenda tu kuwataarifu kuwa sisi huenda huku bungeni mshahara tukapandishiwa kwa hiyo kwa kasi furani sishawishingi kivilee kuzungumzia maslaihi yako kwanza mwangu hasomi huko hizo ni shida zako (hayo ndo matamko ya mbunge rohoni kwao japo mdomoni wansema kwa kifupi tu serikali itatue matatizo ya waalimu)
   
Loading...