surubu kwetu
Member
- May 13, 2014
- 59
- 12
Leo ikiwa ni Siku yangu ya kuzaliwa ningependa japo kidogo nizungumzie kuhusu Tanzania yangu.kabla ya yote napenda kuweka wazi Itikadi na msimamo wangu Mimi sio mwanachama wa chama chochote cha siasa Tanzania ila huwa nimfatiliaji wa siasa za Tanzania na duniani kwa ujumla baada ya kusema hayo napenda niende kwenye Maada yangu
TANZANIA.
Tanzania yetu kumekuwepo na malalamiko mengi sana kutoka kwa makundi mbalimbali kama vile vyama vya siasa,wanaharakati,viongozi wa dini,asasi za kiraia.Sababu zao kubwa ni kuhoji upatikanaji wa uhuru, haki,vitendo vya utekwaji wa watu na vitendo vingine.Hapa ntazungumzia kwa njia mbili tofauti
1:Kuunga mkono serikali kwa mambo kadhaa
Kwanza:Nakubaliana na Sera ya kujenga viwanda-mimi kama kijana Mtanzania natamani kuiona Tanzania ikiwa ya viwanda sisi kama watazania tukijenga viwanda vingi tutaongeza uwezo wa nchi kujiendesha yenyewe na kuongeza ajira nyingi sana
Pili:Nakubaliana na serikali kwenye ujenzi wa Miundombinu kila mmoja wetu amekuwa akiona jinsi ujenzi unavyoendelea kama Barabara,reli na viwanja vya ndege.
Tatu:Nakubaliana na serikali kwenye ujenzi wa bwawa la kuzalisha umeme kwenye ili lazima sisi kama watanzania bila kujali misimamo yetu tuungane kwa pamoja tukifanikiwa kuzalisha umeme wetu wenyewe tutapunguza gharama za umeme na lengo la tanzania ya viwanda litatimia.
2:Sikubaliani na serikali kwa haya.
Kwanza:Kutoweka Itikadi zao pembeni-kwa hili uwenda walio wengi hawalioni ila ni jambo hatari kwa nchi leo kiongozi fulani anasimama mbele ya wananchi nakusema usipochagua chama changu atuwaletei maendeleo hivi kiongozi unalipwa na pesa ya walipa kodi watanzania unaweka itikadi mbele kwa maendeleo ya taifa unaweka chuki kwa watu hasara yake ni kubwa sana.
Pili:Kutotii mamlaka kwa sasa viongozi wengi wa serikali kiukweli tena wa kisiasa awatii sheria kabisa leo viongozi anasimama nakupiga marufuku upinzani kufanya kwenye eneo lake najiulizaga hivi hizi sheria ziliwekwa kwa ajili ya wakina nani? Wengine wanasema atamshangaa mkurugenzi wa uchaguzi kumtangaza mpizani kama mshindi hivi anafikiriaga kweli? Hili no hatari kwa taiga letu kama tunataka tuwe wazalendo basi tukubali kukosolewa ili tujenge umoja wetu.
Tatu:Kutowapa wabunifu kipaumbele-nimekuwa naumia sana kuona vijana wengi wanakuwa na project nzuri kabisa ila serikali awayapi uzito wa kutosha mfano wanafunzi wengi wa chuo wana project nyingi sana ila akuna msaada wanaopata ili tuwe na taifa linaloweza kujitegemea lazima tuwe na wabunifu wetu wenyewe ivi tutajenga viwanda bila kuwa na wabunifu na wanasayansi wetu wenyewe? Ikitokea tukawekewa vikwazo je tutafanyaje?
Mwisho:Ushauri na maoni yangu
1:serikali lazima iwawezeshe vijana wabunifu wa kitanzania kwa mfano inaweza kujenga mji au kijiji maalum kwa wanasayansi na wabunifu wa kitanzania na liwe na ulinzi mkali ili kulinda haki miliki ya wabunifu wetu wanaweza kuandaa sheria jinsi gani wanaweza kuwapata.
2:Nchi yetu inaitaji tasisi imara sio mtu moja ndio anakuwa na mamlaka je tukipata mtu ambaye sio muadilifu itakuwaje.
3:kuwepo na umoja wa kitaifa tutengezeneze maridhiano uchaguzi ukiisha tukae kama taifa tuangalie tunataka nini kama taifa hivi Kenya wameweza,Zanzibar waliweza kwanini tushindwe?