Dotto, baada ya kusoma kwa makini hoja yako, nimegundua maneno matatu kama ifuatavyo:
Kwanza, kama kweli wewe ni mwandishi wa habari ulivyojitambulisha, basi utakuwa kanjanja. Nasema hivyo kwa sababu nimegundua uelewa wako wa mambo yanayotokea duniani ni mdogo kupita kiasi hata kile kinachotakiwa kwa mwana habari mwanafunzi. Haihitajiki darubini kupima na kuelewa kwamba TBC ni shirika la umma linalogharamiwa kwa kodi ya wote bila kujali itikadi, dini wala jinsia za watz.
Kwa mukhtadha huo, chombo hicho kinapaswa na hakika kinawajibika kuwa fair kwa wote bila kujali dini wala itikadi. Lakini ukweli ni kinyume chake inapofikia suala la kuripoti habari za CCM na vyama vingine vya upinzani. TBC hujikuta wakiripoti habari za CCM kama ilivyotakiwa kuripoti Radio au gazeti la Uhuru ambavyo ni vyombo vya propaganda vya CCM
Tema hali imekuwa mbaya zaidi baada ya Clement Mshana kurejea TBC kama Mkurugenzi. Ukereketwa na uelewa mdogo wa Mshana ulidhihirika kwa kipindi kifupi alichokaa Idara ya Habari Maelezo ambapo alitumiwa na CCM na serikali yake kujaribu kudhibiti uhuru wa vyombo vya habari kwa kuviandikia barua za onyo, karipi au kusudio la kuvichukulia hatua magazeti yaliyoripoti habari za ukweli ambazo hazikuwafurahisha watawala. Yaliyotokea utakuwa unayajua kama kweli wewe ni mwandishi wa habari.
Jambo la pili nililogundua ni kwamba uwezo wako wa kujenga hoja ni mdogo. Haki siku zote huenda pamoja na wajibu. Je, kama waandishi wa habari wa TBC wana haki ya kuhudhuria na kuripoti habari za makundi yote katika jamii, basi pia wanayo wajibu wa kuzingatia taaluma, ukweli na ueledi katika utendaji wao. Wasitumike na CCM, Chadema, TLP, NRA, NCCR-Mageuzi...........nk.
Tatu na mwisho, kwani ni lazima waandishi wa habari wafuatilie na kuripoti habari kutoka kwa source asiyewahitaji. Kwanini TBC wang'ang'anie kwenda kwenye matukio ya Chadema wakati wahusika hawawahitaji? Lazima wawe na hila iliyojificha, nalo siyo lingine bali 'KUWALIMA' kwenye story
Nakushauri usionyeshe uwezo wako mdogo au mishiko unayopata kutoka CCM kupitia kwa bosi wako anayekufundisha kazi (kutoka moja ya vituo vya Tv nchini) ambaye ni roboti ya kufanikisha baadhi ya mapenzi ya wana CCM kudhalilisha fani ya habari kwa kuleta jamvini hoja zisizo na mashiko. TBC waache kulazimisha kuhudhuria matukio wasiyotakiwa wala kualikwa, habari ziko tele siyo lazima za Chadema. Kuna vyama zaidi ya 17 vya siasa nchini na kingine kipya kiko njiani wacave huko.