Maoni yako katika utata huu

Maoni yako katika utata huu

Mukwano jebaleko

JF-Expert Member
Joined
Mar 30, 2015
Posts
402
Reaction score
214
Ndugu watanzania wenzangu kumekua na tabia ya wanatanzania wengi sana kutumia lugha ya kiswahili na kiingereza katika mada ambayo imeanzishwa kwa lugha ya kiswahili....au mtu anahojiwa kwa kiswahili lakini anajibu kwa kiingereza na hali akijua kuwa ni mtanzania na wanaomsikiliza ni watanzania tena wakati mwingine hata hawajui kiswahili...Je unadhani ni nini chanzo cha utata huu?toa mtazamo wako ili tuelimishane katika hili...

Mukwano
 
Wengi wao ni washamba,wanadhani kupiga kiswa-kinge ndio utaonekana msomi au ndio utaonekana umekaa sana majuu.
 
Profile picture yako inamaneno ya kingereza.. unaonaje ingekuwa kiswahili tu?
 
Wi-fi tatizo ni kuchanganya lugha, mada au majidiliano ni ya kiswahili we unajibu kwa kiswa-kiinge!profile yangu haijachanganya lugha kaka nimetumia lugha moja....na ishu ni kwenye majadiliano au malumbano ya hoja
 
Wengi wao ni washamba,wanadhani kupiga kiswa-kinge ndio utaonekana msomi au ndio utaonekana umekaa sana majuu.

Kwa hiyo unataka kusema wanataka kutambulika kama nj wasomi kupitia id ya Kiswa-kinge?na je unadhani hiyo dhana ni nzuri?
 
Hivi ishu ni kiswahili au kingereza mbona mtoa mada unajichanganya
 
Kabixa huo ni ushamba na wandewazimu usio na kichwa cha mbele wale nyuma unakuwa msaliti wa lugha yako ya taifa
 
Wi-fi tatizo ni kuchanganya lugha, mada au majidiliano ni ya kiswahili we unajibu kwa kiswa-kiinge!profile yangu haijachanganya lugha kaka nimetumia lugha moja....na ishu ni kwenye majadiliano au malumbano ya hoja

Wi-fi, profile, ishu. Hayo maneno yote yana kiswahili chake ila wewe umeyaweka kwenye maelezo ya kiswahili...hapa unajijadili mwenyewe bila kujijua!
 
wewe ukiwa rahisi utapiga marufuku watu kuongea kiingereza kabisa maana uba roho mbaya mno

#Zitto
 
Kabixa huo ni ushamba na wandewazimu usio na kichwa cha mbele wale nyuma unakuwa msaliti wa lugha yako ya taifa

Yaani bora hao wanaochanganya lugha kuliko nyinyi mnaoandika kabixa badala ya kabisa!..nyinyi ndio wapuuzi msiojielewa kabisa
 
Hebu jaribu kuelewa mada ndugu...mada ni matumizi ya kiswa-kinge.ukiangalia profile yangu ina kiswa-kinge?kama umepewa mada ya kiswahili uchangie basi tumia lugha ya kiswahili na si kuchanganya kiswahili na kiingereza vivyo hivyo kama mada ni ya kiingereza basi jadili kiingereza mwanzo mwisho.....
 
Kabla ya kuchangia ni vizur kusoma mada vizuri kwanza.
Me nadhani ni katabia ka kuiga wakenya kamezoeleka hadi kuonekana kama fasheni kuchanganya lugha hizo mbili
 
Back
Top Bottom