Maoni ya watanzania walioko ughaibuni yatakusanywaje?

Kiwi

JF-Expert Member
Sep 30, 2009
1,054
2,000
Heshima zenu wakuu,

Nikiwa mmoja wa watanzania wanaoishi ughaibuni ningependa kupewa maelekezo kutoka kwa yeyote mwenye kufahamu namna gani nasi tunaweza kushiriki katika kutoa maoni yetu hususan kuhusu katiba mpya.

Kuna mpango/mipango yoyote ambayo imefanywa ya wanatume hao kufanya ziara nje ya nchi kukusanya maoni au kuna mtandao wowote au 'forum' ambayo wanaweza kuitumia kukusanya maoni yetu? Ama sisi tulio nje ya nchi ndiyo hatuhusiki kabisa na zoezi hilo lote?

Kwa maoni yangu nasi pia tuna haki kama watanzania wengine angalau kusikilizwa hata kama mawazo au maoni yetu yatakuja kuonekana hayafai, lakini haki ya kimsingi ya kutoa maoni nadhani tunayo. Binafsi ninayo maoni kadhaa ambayo ningependa kuyawasilisha endapo nitapata njia muafaka ya kufanya hivyo. Na ninaamini kabisa ya kuwa siko peke yangu.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom