MAHANJU
JF-Expert Member
- Aug 26, 2014
- 5,244
- 7,970
Kuna wanaosema kua jamaa ana mawasiliano ya siri na aliyekua katibu mkuu wa Chadema Dr Slaa,kwahiyo anamshauri kua chama kwa sasa hakipo salama tofauti na zamani baada ya ujio wa Lowassa! hivyo anamshauri kuangalia njia nyingine ya kujipanua kisiasa mapema zaidi kama kijana"Unajua Mnyika alikua ni kati ya vijana watiifu kabisa kwa Dr Slaa na ndiye alikua Role modal wake wa kisiasa, sasa Dr Slaa hayuko Chadema, inawezekana hawa watu bado wana mawasiliano ya siri na ya karibu sana"haya yalikua ni maoni ya mdau wa karibu kabisa na viongozi wa juu wa chama.
Kuna wanaosema kua kuna uvutano wa kiutendaji kwa shughuli za ndani ya chama na baadhi ya viongozi waandamizi wa chama,kwa upande mwingine kuna wanaosema kua John Mnyika ni kiongozi makini asiyeyumbishwa na mtu yeyote nje na ndani ya chama, hivyo ukimya wake unaweza ukawa na nia njema kukijenga chama zaidi kuliko uvumi wa kwenye vyombo vya habari.
Kuna wanaosema kua Mnyika kutokana na kujihusisha kwake na siasa tangu akiwa mwanafunzi chuo kikuu kulimfanya kupata mizengwe mingi iliyomharibia masomo yake na kumpelekea kutofanikiwa kumalizia masomo yake ya chuo kikuu, hivyo huenda kwa sasa anamalizia shule yake na ukizingatia pia anayo majukumu ya kuhudumia wananchi ndio maana ameamua kupuuzia propaganda chafu dhidi yake kwenye media
My take;
kama kuna ukweli wowotete kati ya michango au maoni ya wadau hao, na kwa kuzingatia nafasi ya Mnyika ndani ya Chama ni bora kuwatoa hofu wananchi wanaojiuliza maswali mengi juu ya ukimya wake, sidhani kama kujitokeza kwake hadharani kuzikanusha propaganda hizo chafu zinazoenezwa dhidi yake kunaweza kumpunguzia lolote kwani anafahamu siasa za nchi hii zilivyo.