Maoni kutoka Mzalendo net.

simplemind

JF-Expert Member
Apr 10, 2009
16,418
9,206
mzeekondo 31/03/2017 kwa 3:51 um · Log in to
Reply
Hivi karibuni niliwahi kuandika kidogo “scenario”
niliyoiona ambayo kuna uwezekano mkubwa
tukafika huko,ikiwa huu unaoitwa mgogoro
utafanikiwa kutuletea matokeo tusiyo
yatarajia,katika mkanda huu wa leo wa
mhashimiwa Tundu Lissu,nae pia amegusia yale
yale ambayo niliyanena awali, kuwa wanasubiri
kwa hamu mpango huu ufanikiwe, ili iwe neema
kwa upinzani,hapa ndipo nina poshindwa
kuwaelewa kina Balozi Iddi na wenziwe
wanaousuka mpago huu,kwa kutumia gharama
kubwa huku wakisaidiana na Lipumba, ili
kuimaliza cuf na Maalim Seif kwa mawazo yao.
Tatizo liko hivi,CUF sio jengo au chama, ni
WATU, sasa hata kama ccm tukifanikiwa kukiuwa
chama hiki cha wananchi{cuf}kwa hapa
Zanzibar,hawa wanachama wao wa miaka yote
hii wanao tusumbua kila uchukuzi/uchaguzi ukija,
ghafla ndio watakuwa watu wetu, na watakipigia
kura chama cha mapinduzi na wagombea wetu
wote?
Jawabu ni hapana,sasa kwa nini tunapoteza
nguvu nyingi na muda wote kukifuta chama
ambacho hata kikitoweka duniani leo, bado sisi
tatizo letu halijakoma?huu ni uwenda wazimu wa
kisiasa,tusichanganyikiwe kiasi hiki baada ya
kukataliwa kwa kishindo katika uchaguzi halali
uliopita wa oktoba 25.2015,mpaka tukadhani
“solution” ni kukiuwa chama cha CUF,huku ni
kujipalia makaa.
Turudi nyuma na tuimie historia kidogo,ccm kuna
wakati tulimtumia Zitto Kabwe ili akiuwe au
akichafue chama cha chadema, na tuliitumia
pesa nyingi na mahamaka kumhalalishia ubunge
wake baada ya kufukuzwa na chadema,hatimae
akaendelea na ubunge na kuamua kuanzisha
chama chake binafsi cha siasa ACT {alliance for
change and trasparency, yaani umoja wa
mabadiliko na uwazi}hivi sasa bado mbunge kwa
tiketi ya chama chake na yuko bungeni
anawakilisha jimbo lake.
Mara kadhaa inapobidi yeye binafsi hujiunga na
wapinzani katika kuiweka msalabani ccm ndani
ya bunge,tatizo lengo letu la kukiuwa au
kukichafua chadema tulivyo kusudia
haikuwezekana, badala yake ndio tukapata
upinzani wa hali ya juu, ambao haukuwahi
kutokea katika uchaguzi uliopita, kwa mara ya
kwanza tangu kuanzishwa kwa vyama vingi,
mgombea wa urais wa upinzani wa chadema
Lowassa, alipata kura millioni zaidi ya sita baada
ya kuzipunguza, na yule wa ccm Magufuli
alipewa millioni zaidi ya nane huu ndio
ukweli”facts”
Ninachotaka kukisema hapa,ni lazima tukubali
hatuna hiari haya tunayofanya sio uungwana
wala sio demokrasia,huu ni uhuni wa kisiasa na
huu hufanywa pale utawala unapokuwa hauna
watu tena wa kuwaunga mkono,hapo ndio
hutumika nguvu za dola na mikakati ya ovyo
kama hii, ili kujiweka katika uongozi
tusiostahiki,hili nalo kuna wasomi watabisha,
msibishe ovyo leteni vigezo”data” mdomo mtupu
sivyo mlivyosomeshwa na kuhitimu, na kwa wale
vichwa viwazi kama mimi utawalaumu vipi? na
wao hawana wanachokielewa.
Maalim Seif kwa nilivyo msoma kwa miaka
kadhaa sasa, nina imani anaelewa nini kinaweza
kutokea huko usoni kuhusu mgogoro huu wa
cuf,na yeye ameshajipanga kwa mabadiko ya
aina yoyote kuhusu muelekeo wa kisiasa wake
binafsi na umati wake wa cuf unaomuunga
mkono,Lipumba hana chama wala watu katika
cuf hili linaeleweka, yeye na Zitto Kabwe kama
alivyokuwa chadema anaweza kuondoka na
kuanzisha chama chake, ambacho
kitamhakikishia ruzuku anayo ipenda tu, sio
kingine,na kama atafanikiwa kukiuwa cuf kwa
msaada anaoupata kutoka kwa Magufuli,msajili
wa vyama vya siasa na mahakama, basi atabakia
na chama cha cuf kama jina, pamoja na majengo
yake, hasa lile la pale buguruni, lakini watu
hatowapata,wote watakwenda kule alipo kiongozi
wao wanae muamini, yaani Maalim Seif,sasa nani
anajua wapi maalim ataelekea? suala ni
wapi,nahakika harudi CCM.
Chadema kina nguvu Tanganyika kama CUF ilivyo
hapa Zanzibar,Ukawa imewafunua macho
wapinzani hawa wawili na kujua, ili kuiondoa na
kukabiliana na CCM, ni lazima wafanye kazi kwa
kushirikiana,pamoja na kubadilishana
mawazo,hivyo vyama vingine vingi unavyo visikia
vya siasa hapa Tanzania, ni wasindikizaji na
watafuta ruzuku tu.
Vyama hivi havitaki kuungana kwa hiari yao, kitu
ambacho kingekuwa kizuri kimikakati,
kidemokrasia na kuleta ushindani wa vyama
tunao utarajia, bahati mbaya wala hawana mpago
huu,lakini serekali ya ccm inafanya kila inalo
weza, kuwa unganisha kwa nguvu bila kujua, sijui
kwa faida ya nani?sidhani kama ni ya ccm,sasa
ikiwa kuungana kwao ndio mauti ya ccm, basi
msajili wa vyama vya siasa,mahakama,Magufuli
au ccm mpeni chama cha cuf Lipumba, halafu
muone kama 2020 ikulu zote mbili ya bara na hii
yetu hapa Zanzibar, marais watakao hamia humo
watakuwa Lipumba na Makufuli.
Sio kila unachoomba unapata,omba chenye kheri
peke yake, na mtangulize Mola kwanza, kila
ukijaaaliwa.
Inshaalah Zanzibar itakomboka.
 
Back
Top Bottom