Maoni Katiba mpya Dar moto

R.B

JF-Expert Member
May 10, 2012
6,296
2,573
[h=2] [/h] MCHAKATO wa kutoa maoni kwa ajili ya Katiba mpya mkoani Dar es Salaam, umeanza kwa kasi ya aina yake, baada ya jana suala la ugaidi kuibuka. Katika mkutano huo, waumini wa dini ya Kiislamu waliilalamikia Serikali na jamii, kwa kuwahukumu kuwa wanahusika kwa asilimia mia moja katika vitendo vya kigaidi.

Waislamu hao, walitoa kilio hicho jana katika Viwanja vya Buriaga, wilayani Temeke.

Imamu wa Msikiti wa Temeke, Hamed Suleiman Hamed, alisema sheria iliyopo ya ugaidi, imelenga kuwadhalilisha Waislamu ndani ya jamii na nchi yao, hali ambayo inafikia kiwango cha kutoaminika sehemu yoyote.

Alisema ni vema Katiba mpya, ikakifuta kipengele hicho kinachosababisha wanapovaa mavazi na kufuga ndevu, basi inakuwa ni tiketi ya kushiriki ugaidi.

Naye Aisha Suleiman aliunga mkono kauli hiyo na kusema kitendo cha Waislamu kufunga ndevu ndefu na kuitwa magaidi si cha kiungwana.

“Ni vyema kwa katiba mpya inayoandaliwa kukifuta kipengele cha kuwaita Waislamu wanaofuga ndevu magaidi, kwani kufuga ndevu kwa Waislamu ni suala la kufuata sunna ya Mtume (S.A.W),” alisema Suleiman.

Katika mvutano huo, kila kundi lilipendekeza maoni yake juu ya mavazi na mwisho wakapendekeza katiba mpya isiruhusu mavazi ya vyama vya siasa.

“Uanzishwaji wa sare za vyama vya siasa, umeonekana wazi kuwagawa Watanzania na kuleta uhasama, chuki na hata kusababisha mauaji, baada ya kutofautiana kiitikadi.

“Ni vyema tukajifunza kupitia uchaguzi wa Marekani, hakuna mwananchi aliyeonekana na sare ya chama, bali wote walikuwa wakipeperusha bendera ya nchi yao.

“Kama kipengele hicho hakitakuwepo katika katiba mpya itakayokuja basi Watanzania wataendelea kugawanyika makundi na nchi haitakuwa na amani, upendo na utulivu na badala yake tutaingia kwenye vita ya wenyewe kwa wenyewe,” alisema Kafuru Kapuma.

Katika maoni mengine, wananchi wa Temeke walipendekeza Katiba mpya ijayo kuwepo na kipengele cha Rais kushitakiwa, kupunguziwa madaraka, asiteue majaji, kufutwa kwa viti maalum na wabunge wa kuteuliwa.

Mengine ni kumuondolea mbunge kinga ya kumfungulia shitaka kama amesema neno la uongo bungeni, kuwapo na uwiano wa ajira kati ya Wakristo na Waislamu na shule zirudi katika mfumo wa zamani wa kutenganisha jinsia, huku wakisisitiza Kiswahili kitumike kufundishia.

Katika hatua nyingine, walipendekeza Bendera ya Taifa ibadilishwe rangi kwa kuondoa rangi nyeusi na kuweka nyekundu, ambayo itaonyesha Watanzania wapo kwenye mapambano ya kuokoa nchi yao.
 
Hapo kwenye vaz la chama wamechemka,gwanda ni vaz la heshma sn,nalipenda kupita maelezo.
 
Kwenye kiswahili kuwa lugha ya kufundishia wanachemka tutazidi kuwa nyuma maana sayansi hamna uswahili pale...ni ngeli mwanzo mwisho
 
mie wameniacha hoi kwenye suala la kubadilisha rangi ya bendera , nyusi na kuweka nyekundu hapo ni tatizo tayari. maana ya rabgi nyekundu ni umwagaji wa damu.
inamaana kuna damu inategemewa kumwagika soon.
jamani tuwe macho hapo
 
Back
Top Bottom