MAONI BINAFSI: CCM waitishe maandamano ya amani kupinga kuporwa ushindi wao

ngusillo

JF-Expert Member
Nov 5, 2019
1,068
2,000
Turejee uchaguzi wa serikali za mitaa.

Mpaka jana, CCM walikuwa na ushindi mnono wa asilimia 90. Ushindi huu ulikuwa kwenye ngome za wapinzani, mfano Kilimanjaro, Dar es Salaam, Mara, Manyara, Kigoma, Mbeya na kwengineko.

Ilichokuwa imebakisha CCM ni kwenye ngome zake ambako ushindi wa asilimia 100 ulikuwa guaranteed.

Ghafla leo jioni waziri wa Tamisemi Suleiman Jafo, anaamua kuingiza uwanjani wachezaji waliopewa
Red Card kwenye mchezo huo huo, masaa machache yaliyopita.

Niwashauri CCM wakatae hila hizi za Mh Jafo. Waandamane nchi nzima kudai haki zao zinazoporwa kwa maslahi ya wahalifu wachache wasiojua kujaza form.

Nimtake katibu mkuu Dr Bashiru atoe tamko usiku huu, ili kukipambazuka tuingie barabarani.

Kwa kuwa sisi ni chama tawala, naamini polisi watayalinda maandamano yetu ya amani na tutaweza kuuonyesha uma jinsi tunavyokubalika na Rais wetu anavyokubalika.

Ni hayo tu.
 

ngusillo

JF-Expert Member
Nov 5, 2019
1,068
2,000
Kwani nyinyi mumejenga reli mumujenga madaraja mumenunua ndege lkn munaogopa jambo dogo tu uchaguzi wa huru na haki
Hatuna muda wala pesa za kupoteza kwenye uchaguzi. Tulishashinda kwa 98%, zilibakia 2%. Lakini tunamwona Jafo anazunguka huko na huko akijaribu kuwapa penati za bure upinzani.

Hatukubali. CCM mbrle.na nyuma.
 
Top Bottom