Maongezi yangu na Daktari wa Muhimbili leo | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Maongezi yangu na Daktari wa Muhimbili leo

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Donn, Jun 23, 2012.

 1. Donn

  Donn JF-Expert Member

  #1
  Jun 23, 2012
  Joined: Jun 5, 2012
  Messages: 2,451
  Likes Received: 38
  Trophy Points: 145
  Kwanza niliuliza juu ya sababu za mgomo. Na zifuatazo zilikuwa moja ya sababu

  * Miaka iliyopita kila wodi ilikuwa na mahabara na mgonjwa akifikishwa anapata vipimo na huduma maramoja. Lakini leo hii mtu wa ugonjwa wa kansa anatakiwa kusubiri mpaka miezi miwili ili kupata majibu. Hii ikitokana na maabara nyingi kufa. JE TUNATEGEMEA WAGONJWA HAWA KUPONA?

  * Kutokana na ukosefu wa dawa, wagonjwa wenye ugonjwa mmoja ambao dawa zake hazipo hospitali huandikiwa dawa huku baadhi ya dawa hizo kuwa na gharama sana. Ni wazi kuwa yule mwenye pesa atapona na masikini atakufa. Hili ni pigo kwa daktari kwani hayupo pale kutazama watu kufa bali kuwaokoa.

  NA MENGINE MENGINI ALIYASEMA.

  Lakini leo tunawatazama kama watu wasiotutakia mema. Mtu anayeng'ang'ania dawa kuletwa ili upone leo anapondwa na wasio uwezo wa kutafakari.

  SINA UWEZO WA KUINGILIA AMRI YA MAHAKAMA, ILA NINGEPENDA PIA SHERIA IPITISHWE ILI VIONGOZI WOTE WATIBIWE NCHINI TU. Hapo tutaenda sawa

  Ni mtazamo tu... Peopleee....
   
 2. e

  ellyjr8 Member

  #2
  Jun 24, 2012
  Joined: Jun 23, 2012
  Messages: 56
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  UKWELI KUHUSU MGOMO WA MADAKTARI TANZANIA.
  MADAI
  1. Kuboresha Huduma za afya hospitalini kwa vifaa vya upimiaji, madawa.
  2. Kuboresha Mazingira Ya kazi (ukarabati wa majengo, uongezaji wa vitanda)
  3. Posho ya muda wa ziada wa kazi (call allowance) 5% kama ilivyo kisheria kwa kada yoyote.
  4. Posho ya kufanya kazi katika mazingira magumu 40% ( MEANING anayefanya kazi SAME, TANDAHIMBA, NYAMPULUKANO nk ni tofauti na akaaye MJINI)
  5. Posho ya makazi 40% au nyumba kama ilivyo kisheria(since DOCTOR IS ENTITLED KUPATA, HII NI KATIKA SHERIA YAO WENYEWE)
  6. Bima ya Afya(Green Card) kwa wafanyakazi wote wa sekta ya Afya.
  7. Kuwaondoa viongozi wa juu wa W/Afya kutokana na ubadhirifu.
  8. Posho ya kufanya kazi katika mazingira hatarishi 30% au Chanjo(Homa ya ini-hepatitis, HIV/AIDS, TB)

  MAKUBALIANO
  1. Kuondolewa kwa viongozi na watendaji wa juu wa Wizara ya Afya
  2. Kupewa nusu ya ombi la call allowance hadi pale baada ya mazungumzo(ktk kipindi cha mpito)
  3. Kamati kujadili na kuona kiasi gani mshahara na posho zitaongezwa kwa kutengeneza(developing a formula)
  4. Serikali kuongeza bajeti ya W/Afya ili kuongeza vifaa, na madawa.

  HALI ILIVYO SASA
  - HOSPITALINI: hakuna huduma za afya (matibabu, upimaji wala upasuaji), YAANI NI KWELI TUMEGOMA
  - VYOMBO VYA HABARI: Kuna upotoshwaji mkubwa wa taarifa kwa umma.
  - MTAANI:Hofu na mashaka kwa wananchi kutokana na kutoelewa matamko yanayopingana kati ya Serikali na Tamko la madaktari

  MTAZAMO
  HEBU ANGALIA KATIKA MAKUBALIANO NI LIPI LIMETEKELEZWA HADI SASA?? THEN SERIKALI INAONGEZA MISHAHARA YA WABUNGE, HIVI KARIBUNI UTASIKIA SABASABA!!!
  - Jumla ya madaktari wote ni chini ya 15,000 (na hapa namaanisha General practitioners and Specialists). Kwa uchache au wingi wetu tumekwisha kuona madhara ya migomo miwili iliyokwishatokea.Nashangwazwa na kuona baadhi ya watu wanaosema madaktari hatuna utu wala huruma na tunaweka maslahi yetu mbele, hivi mnajua kuwa katika nchi za East and Central Africa, Tanzania ndiyo yenye kulipa mishahara midogo kwa watu wa sekta ya Afya?? Rwanda juzi juzi(1994) walikuwa na vita lakini daktari analipwa 1500USD, au mnadhani hatujui kuna nchi za jirani na mbali tunaweza kwenda kama wenzetu (Mf. Rwanda, Botswana, Zambia, Lesotho, Egypt, SA, nk)???mnadhani kubaki kwetu Tanzania tuteseke kwa kauli eti "UDAKTARI NI WITO?", "WATANZANIA -WATOTO, KINA MAMA, NA WAZEE WATAKUFA IWAPO TUKIGOMA", "OOOH?? HATUTAKIWI KUGOMA"…tumeonyesha uzalendo wetu kwa kubaki hapa hapa na mazingira yetu magumu, lakini sasa IMEFIKA MWISHO..
  Pediatrics(wodi ya watoto):Hakuna vifaa vya kuongezea maji/damu mwilini(cannula), hakuna mitungi ya gesi, OBGYN(wodi ya kina mama);hakuna pamba, mipira ya mikojo(urine bags), MOI, Mwaisela hakuna vitanda, Operating Theatre,OT; Hakuna gloves ,mask, kofia za kutosha, Huduma ya mionzi ya CT SCAN ni mwezi wa saba haifanyi kazi(huku mmiliki akiwa anaidai Wizara ya Afya mil.800/=Tsh)na haitakuwepo hadi atakapolipwa.
  Kwa madai hayo, si lazima serikali itekeleze all at once, lakini Mshahara unazungumzika, wale mnaofanya interview, huwa hamuulizwi ni kiasi gani unategemea kuanza nacho na waajiri wenu? Doesn't this make salary being negotiable?? Then kwanini isiwe kwetu?
  Hivi ulishawahi kusikia MASS RESIGNATION????? It takes ATLEAST 12yrs kumpata huyo specialist after elimu ya sekondari, Halafu nasikia mnasema eti tufukuzwe kazi?Then what??? Kwa wale wenye mtazamo mfupi mnadhani Serikali inaweza ku-import madaktari toka nje..kwa mfano
  1.Ni nchi gani itakuazima madaktari?? Kwa mshahara upi na vifaa gani? CUBA-3000USD, RWANDA-1500USD!!!
  2.Hypothetically speaking, wakikusaidia madaktari, watakupatia wangapi??
  3.Apartment na transport allowances utawapa kiasi gani?
  4.Hivi bibi aliye Tandahimba, asiyejua Kiswahili vizuri ataweza kuongea kiingereza na hao doctors??ama utahitaji wakalimani(translators), if so wangapi??? Utawalipa??
  5.Then hao madaktari watakaa hapa milele??
  Then NASIKIA MTATUPELEKA MAHAKAMANI.
  Utawakamata madaktari wote nchini?? Kumbuka huu mgomo hauna kikomo na hauna kiongozi!!!..hypothetically speaking ukitupeleka, tutawatibu tukiwa huko gerezani?? Waliobaki mnadhani watarudi makazini?tukirudi mnadhani tutafanya kazi? Tukifanya kazi unadhani itakuwa katika kiwango kinachotakiwa? With demoralization unategemea tutaponyesha ndugu zetu kweli, au mortality kuwa juu??? Then kwa wanafunzi walio vyuo vya tiba kama MUHAS, WBUCHS, KCMC, UDOM, HKMU, IMTU..watafanya kazi hapa nchini kwa hali hii, ama Brain drain ndiyo itazidi!!
  SIASA.
  Wananchi walishazoea kudanganywa, na hii imezoeleka na viongozi Fulani kushindwa kufanya wajibu wao kusingizia wanasiasa kadhaa..Hapa HAKUNA siasa ila mkiileta tutawaachia tu kwani huko hatupawezi ila viongozi mjue hakuna tena rufaa ya kwenda nje(mf. INDIA) MUHIMBILI
  Hivi wananchi mnajua viongozi wanalipwa kiasi gani wanapoenda nje kutibiwa na familia???
  Eti kwa sababu sekta nyingine hawawezi kugoma, ndio na sisi tusigome? Eti kwa sababu askari anayetumia SMG na kupambana na jambazi anayetumia AK47, eti kwa sababu mishahara ya walimu inacheleweshwa, ndio tusigome??? Nani kasema??
  HITIMISHO:
  HAPA KAZINI HATURUDI…HII IELEWEKE VIZURI…HATURUDI….MGOJA NIIWEKE VIZURI HATURUDI, ACHA MEDIA IENDELEE KUDANGANYA, LAKINI UKWELI TUNAUJUA, MWISHONI MTARUDI TU, NA THIS TIME SI TENA YA KUTUMIA BUSARA ZETU KUWASTAHI VIONGOZI NA KISHA KWENDA PALE KUONGEA NA ‘WAZEE WA DSM"
  "Doctors we might be slow walkers, but we never walk back" ..Solidarity Forever
   
 3. R

  Ray2012 JF-Expert Member

  #3
  Jun 24, 2012
  Joined: Apr 1, 2012
  Messages: 215
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  uwongo utajitenga, ukweli utabaki!
   
 4. Donn

  Donn JF-Expert Member

  #4
  Jun 24, 2012
  Joined: Jun 5, 2012
  Messages: 2,451
  Likes Received: 38
  Trophy Points: 145
  dah.. Ahsante kwa ku add points elly
   
 5. Communist

  Communist JF-Expert Member

  #5
  Jun 24, 2012
  Joined: Jun 1, 2012
  Messages: 5,391
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 135
  Sasa mimi niko hapa muhimbili nimepigwa risasi nisaidieni
   
 6. Christine1

  Christine1 JF-Expert Member

  #6
  Jun 24, 2012
  Joined: Feb 26, 2012
  Messages: 12,297
  Likes Received: 1,216
  Trophy Points: 280
  hiiyo ndo hali halisi!
   
 7. e

  ellyjr8 Member

  #7
  Jun 24, 2012
  Joined: Jun 23, 2012
  Messages: 56
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  yes donn..habari ndiyo hii..hapa wananchi wasipoelewa watakuwa wamejipanga kutoelewa tu!
   
 8. Jackbauer

  Jackbauer JF-Expert Member

  #8
  Jun 24, 2012
  Joined: Oct 28, 2010
  Messages: 5,920
  Likes Received: 89
  Trophy Points: 145
  x ray na ct scanner ni mbovu hivyo ni vigumu kujua risasi iko wapi,labda upasuliwe hivyohivyo mpaka ipatikane.ungeweza kuongezewa damu lakini mifuko ya damu imeisha.pia itabidi uwapigie simu ndugu zako wakanunue dawa ya maumivu hapo nje.
   
 9. Ruttashobolwa

  Ruttashobolwa JF-Expert Member

  #9
  Jun 24, 2012
  Joined: Feb 22, 2012
  Messages: 43,748
  Likes Received: 12,842
  Trophy Points: 280
  Serikali ya wapotoshaji
   
 10. dfreym

  dfreym JF-Expert Member

  #10
  Jun 25, 2012
  Joined: Oct 14, 2010
  Messages: 337
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  kweli kazi ipo
   
 11. N

  Ninaweza JF-Expert Member

  #11
  Jun 25, 2012
  Joined: Dec 14, 2010
  Messages: 7,188
  Likes Received: 1,190
  Trophy Points: 280
  wagonjwa woote watawarifaa india!
   
 12. N

  Ninaweza JF-Expert Member

  #12
  Jun 25, 2012
  Joined: Dec 14, 2010
  Messages: 7,188
  Likes Received: 1,190
  Trophy Points: 280
  Hivi ni kwanin tunapoteza pesa nyingi kuchagua viongozi wakati taifa linaweza kusimama bila kuwa nao kama inavyo dhihiri sasa hivi?
   
 13. mayoscissors

  mayoscissors JF-Expert Member

  #13
  Jun 25, 2012
  Joined: Nov 24, 2009
  Messages: 762
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 35
  serikali imeshikwa pabaya..jk ngoma itakuondoa na pinda wako
   
 14. Tume ya Katiba

  Tume ya Katiba JF-Expert Member

  #14
  Jun 25, 2012
  Joined: Apr 6, 2012
  Messages: 4,892
  Likes Received: 732
  Trophy Points: 280
  Hoja ni maslah au vitendea kazi au waheshimiwa kutibiwa nje? mbona mnayumba madr?
   
 15. m

  mahoza JF-Expert Member

  #15
  Jun 25, 2012
  Joined: Mar 11, 2012
  Messages: 1,242
  Likes Received: 411
  Trophy Points: 180
  I love dis mimi nawaunga mkono. Viongozi mishahara mikubwa haya angalua hao watu wajumbe wahiuo katiba hela wanayopata kwa siku ni balaa.
   
 16. k

  kitenuly JF-Expert Member

  #16
  Jun 25, 2012
  Joined: Apr 1, 2012
  Messages: 336
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kwa kukuelewesha, viongozi au watawala misonge ( mawaziri, wabunge nk) hawajui adha ya matibabu hapa nchini maana wao wakiugua wanatibiwa india, nafasi hiyo iondolewe ili nao wakutane na adha hiyo wanapougua, hivyo we ndo umeyumba na si madr.
   
 17. I

  IPECACUANHA JF-Expert Member

  #17
  Jun 25, 2012
  Joined: Feb 19, 2011
  Messages: 2,127
  Likes Received: 291
  Trophy Points: 180
  Pole sana....natumaini utapata msaada stahili Ili tuendelee kuchangia maendeleo ya nchi yetu.
   
 18. S

  SHEMGUNGA JF-Expert Member

  #18
  Jun 25, 2012
  Joined: Jan 13, 2012
  Messages: 653
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 45
  nahis ni kutokana na viongoz wasio jal maisha ya wananch naunga mkono madr kugoma!
   
 19. gfsonwin

  gfsonwin JF-Expert Member

  #19
  Jun 25, 2012
  Joined: Apr 12, 2012
  Messages: 16,984
  Likes Received: 1,908
  Trophy Points: 280
  iamani na waalim sasa wanaongezeka hapo what do you think? definately itabidi rais ajiuzulu manake atakuwa ameshindwa kuwajibika ni afadhali kuliko hali ilivyosasa hivi. utakuta mashanging yanawekwa mafuta kwenda kuongea nao why hyo mashanging yasiuzwe yote wanunue tuvits tu ili kupata hiyo mashine ya ct scan? Hosp ya mifupa ya Tumbi haina x-ray yakarinia mwaka sasa eti mashne imechakaa so think of umekuja na mgonjwa ni wa ajali siui unaenda kutafuta x-ray manzese kisha ndio umrudishe tumbi kweli are they serious.

  hivi hatuwez sisi kama wananchi kupiga kura ya kutokuwa na imani na raisi wetu kisha tukamtoa madarakani? je nini hatua za kisheria ambazo zinatulinda sisi ili tuwawajibishe walioko madarakani? nauliza jamani sijui na nikipata majibu naingefurah sana
   
 20. Remote

  Remote JF-Expert Member

  #20
  Jun 25, 2012
  Joined: May 20, 2011
  Messages: 14,880
  Likes Received: 1,563
  Trophy Points: 280
  bakwata wazee wa matamko mmeelewa
   
Loading...