Maonesho ya kijeshi yafanyika Urusi;Putin amesema hakuna taifa lolote linaloweza kuwashinda warusi

Econometrician

JF-Expert Member
Oct 25, 2013
16,627
30,607
_95978825_rusputinmosnewafp.jpg


Rais wa Urusi Vladimir Putin amesifu kujitolea mhanga na kujitoa kafara kwa watu wa Muungano wa Usovieti wakati wa Vita Vikuu vya Pili vya Dunia.

Bw Putin alisema hayo wakati wa maonesho ya kila mwaka ya majeshi ya taifa hilo kuadhimisha Siku ya Ushindi ambayo hutumiwa kukumbuka ushindi katika vita hivyo.

Kwa mara ya kwanza, maonesho hayo ya kijeshi yalishirikisha makombora ambayo yameundwa mahsusi kwa vita katika maeneo yenye baridi kali ya Arctic.

Urusi inajenga kambi mpya za kijeshi Arctic.

"Hakuna nguvu zozote zitakazoweza kuwashinda watu wetu," Bw Putin alisema, na kulaani uharibifu na maafa yaliyosababishwa na Ujerumani wakati wa vita hivyo.

Muungano wa Usovieti ulipoteza zaidi ya watu 20 milioni, zaidi kuliko taifa lolote lile wakati wa vita hivyo.

Muungano wa Usovieti (USSR) ulivunjika mwaka 1991.
_95978823_rustroopsmosreut.jpg

Rais wa Ukraine Petro Poroshenko naye alishiriki katika sherehe ya kuweka shada la maua katika makumbusho mjini Kiev.

Aliwaambia wanajeshi wa Ukraine kwamba Urusi inajaribu kutumia maadhimisho ya ushindi huo "kutimiza mahitaji yake ya kikoloni na upanuzi."

"Kremlin bado inajaribu kuiamrisha Ukraine kama ilivyofanya ilipodhibiti maeneo manne ya vita Ukraine miaka ya 1940."

Urusi imekuwa ikishutumiwa na kudaiwa kudunisha mchango wa nchi nyingine katika vita vya kushinda utawala wa Nazi nchini Ujerumani.

Mataifa ya Magharibi yaliiwekea vikwazo Urusi baada yake kutwaa udhibiti wa eneo la Crimea mwaka 2014.

Urusi pia imekuwa ikituhumiwa kuunga mkono wapiganaji wanaopigania kujitenga kwa maeneo ya mashariki mwa Ukraine.
Urusi imekanusha tuhuma kwamba inasaidia waasi hao kijeshi, lakini imekiri kwamba Warusi wa "kujitolea" wanasaidia waasi.

Jeshi la vijana
Miongoni mwa zana za kivita ambazo zilioneshwa Red Square Jumanne, kulikuwa na makombora ya Pantsir-SA ya kujilinda sana ya kutumiwa maeneo ya Arctic.

Kulikuwa na makombora ya Yars RS-24 ambayo yanaweza kurushwa kutoka bara moja hadi jingine. Makombora hayo yanaweza kutumiwa kurusha silaha za nyuklia.
_95978830_rusyarsrs24moscafp.jpg

Makombora ya nyuklia ya Yars RS-24: Maonyesho hayo yamefufua kumbukumbu za maonyesho ya kijeshi ya Muungano wa Usovieti enzi za Vita Baridi

Wanachama wa jeshi mpya la "vijana wazalendo" ambalo linaitwa Yunarmiya, pia walishiriki maonesho hayo kwa mara ya kwanza.

Hafla kuu ilifanyika Moscow, lakini maonesho mengine yalifanyika katika miji mbalimbali Urusi. Miji mingi iliyoandaa maonesho ni ile iliyoathiriwa sana na vita hivyo vya 1941-1945 ambavyo Urusi huviita "Vita Vikuu vya Kizalendo".
_95978831_russailorsafp.jpg


Wanajeshi wa majini wa Urusi: Jeshi la Urusi limekuwa likijisifia kutokana na uwezo wake wa kupigana vita maeneo ya Arctic

"Ili kuushinda ugaidi, na misimamo mikali na itikadi mpya za Nazi, tunahitaji ushirikiano wa jamii yote duniani," Bw Putin alisema kwenye hotuba fupi.
Urusi imekuwa ikitumia silaha zake mpya katika vita vya Syria, ambapo wanajeshi wa nchi hiyo wanasaidia wanajeshi watiifu kwa Rais Bashar al-Assad.

Wanajeshi wa Assad pia husaidiwa pakubwa na Iran.

_95980300_rusparasreut.jpg

Wanajeshi wa miavuli wa Urusi wakati wa maonesho

_95980299_ruspantsirafp.jpg

Makombora ya kujilinda ya Pantsir-SA yakiwa na kamafleji ya rangi nyeupe mahsusi kwa vita Arctic

_95980296_rustanksreut.jpg
\

5911833dc46188455b8b45a9.jpg

59117836c36188eb7c8b45a2.jpg

5911845fc36188c67f8b45d9.jpg

Russian servicemen parade with Tigr-M (Tiger) all-terrain infantry mobility vehicles and Kornet-D1 anti-tank guided missile systems
59117bbfc46188183e8b45a0.jpg

Typhoon-U armored fighting vehicle
59117d26c36188c1798b45b2.jpg

Msta-S self-propelled howitzer
upload_2017-5-9_21-24-33.jpeg

59117fd3c36188a41d8b4620.jpg

Iskander short range ballistic missile systems
1024px-MAKS_Airshow_2013_%28Ramenskoye_Airport%2C_Russia%29_%28521-05%29.jpg

The Pantsir-S and Pantsir-SA systems are the world’s only air defense missile systems capable of maintaining precision firing while on the move
5911868dc46188455b8b45b8.jpg

Pantsir-S combined surface-to-air missile and anti-aircraft artillery weapon system.
5911872ac4618822618b45e5.jpg

The S-400 Triumf, Russia’s most-advanced long-range defense system, which has no equal in the world now: S-400 Triumf anti-aircraft missile system.
591183efc36188e1798b45cb.jpg

A Yars RS-24 intercontinental ballistic missile system
59044521c4618830088b45b8.jpg

fighter Jet Acrobatics 360
Patrouille_Suisse_c-1024x680.jpg
 
Putin si wa kawaida.
Juz J2 alizama Black Sea kwa kutumia Submarine ndogo hivi ya kioo kwenda kuangalia Bonge la Nyambizi lake lilo zama huku chini ya Bahari. Alikuwa amevalia sare za jeshi.
 
Siku zote anayeonesha siraha zake hadharani si mpiganaji
Siyo kwa Urusi. Putin ni makini sana huyo jamaa.
Yote kwa yote inaonyesha Russia materials zimo sana kichwani. Nchi pekee ya Ulaya ambayo unaweza kusema inaweza kuitisha Russia labda Ujerumani.
 
Back
Top Bottom