Rais wa wakulima
Member
- Sep 27, 2015
- 78
- 19
Habari za muda wanabodi wote natumaini ni wazima wa afya njema pole na majukumu ya hapa na pale.bila kupoteza muda kama kichwa cha habari hapo juu kinavyojieleza, nakuja mbele yenu kuomba msaada wa kimawazo na vitendo ili niweze kufanikiwa.
Mimi ni kijana naishi jijini dar es salaam, kilichonifanya nichukue nafasi hii ya kuandika Uzi huu ni matatizo yanayonikabili naombeni mnisaidie ili niweze kuyatatua japo hata nusu yake.
Nilikuwa nafanya kazi kwenye shirika lisilo la kiserikali, kutokana na matatizo ya kiuchumi shirika lilishindwa kujiendesha na kupelekea kupunguza wafanyakazi kitendo hicho kimeniadhiri sana mimi kwani kimeweza kunirudisha nyuma. Kwani hapa nilipo nadaiwa kodi ya nyumba ambayo natakiwa nilipe sina pesa.
Kwahiyo nawaomba wanabodi jambo mnisaidie ili niweze kulitatua tatizo ili maana linaninyima raha sana hata kama kuna mtu anakijisehemu japo cha mimi kuweza kufanya kazi na kufanikiwa kulipa hii pesa ya watu nitashukuru sana. Naomba msaada wenu.
Asante sana kwa ushirikiano wenu.