Maombi kwa Taifa la Tanzania

Maombi kwa Taifa la Tanzania

Wa Busiya

JF-Expert Member
Joined
Dec 21, 2012
Posts
326
Reaction score
67
Mungu mwenyezi, mwenye mamlaka yote, Baba uliyetuumba kwa mfano wako ili tukuabudu katika Roho na kweli: ninakushukuru kwa kuwa bado umetupenda watanzania ambao bado tuko hai. Najua kila binadamu umempa na kumhesabia siku za kuishi hapa duniani! Baba naomba utupe amani ya kweli sasa maana amani ambayo tumeihubiri kama nchi tumjidanganya wenyewe na kukudanya wewe! Uturehemu ee Mungu kwa uongo wetu sote kama watanzania maana tulichosema ni amani kumbe ilikuwa ni nidhamu ya woga! Sasa imefika wakati watanzania wengi wamepata mwamko wa kuwaambia viongozi au watawala mahitaji yao ya lazima na kuwalaumu kwa wizi, uzembe, upendeleo, unyanyasaji, dhuluma, na kila aina ya mateso na dhambi dhidi ya raia maskini!

Baba! Wape hekima kama ulivyompa mtumishi wako Suleiman ili, hasa rais aweze kuingia na kutoka katika kuwahukumu kwa haki raia wa Taifa hili! Wewe unajua udhaifu au ukamilifu wa viongozi wetu kuliko: unajua hali ya maisha yetu ilivyo kuliko viongozi wetu: unajua ukweli kuwa raia wanabambikiziwa kesi au la: Unajua kuwa wapinzani wanaonewa au la: unajua kuwa viongozi wetu wamejilimbikizia mali ilihali raia ni maskini au la: Unajua kuwa viongozi wetu wanapeana vyeo na kzi zenye maslahi mazuri kwa upendeleo au la: unajua kuwa viongozi wetu wamesaini mikataba mbalimbali kwa hila, ulaghai na wizi au la: unajua kuwa watu wanapigwa kwenye chaguzi kwa sababu tu wanataka haki, na mengine yote wayajua. Sasa Baba uhukumu utusamaehe taifa lote maana neno lako linasema dhuluma ikishamiri mafisadi hupata nguvu. Tusahamehe Mungu wetu mwenye kujaa Huruma na Neema! Wasitaka kutenda haki Waanguke na kutoweka katika jina la Yesu! Maana wewe ni Mungu wa watu wa kila taifa, na kabila, na jamaa, na lugha, na dini, na rangi, na nasaba! Basi Mungu simama uturehemu huku hukumu yako ikimkalia mkorofi asiyetaka kutenda haki!
 
siku Mwingilu akimrudia Mungu na CCM wakakubali matokeo basi mambo yote yatakuwa shwari; otherwise mambo ni magumu sana towards 2015. Ni vema nguvu ya Mungu ikapenywa kwa Wassira na Mwigulu ili taifa liokoke.
 
Bwana Yesu aliagiza watu waombe wasiingie majaribuni. Umesubiri hadi majaribu yameingia. Kilichobaki ni kumwomba atupe mlango wa kutokea kama yeye anavyoona inafaa.

Sent from my BlackBerry 9860 using JamiiForums
 
Mungu hafungwi na mazingira. hata kama sikuomba kabla kikubwa ni badiliko ndani ya moyo na toba ya kweli inayoambatana na nia ya kweli ya kuliombea taifa
 
Back
Top Bottom