Maojiano ya kamanda na tundu mahakamani

jacobinho

Member
Feb 10, 2017
6
12
Lissu alimuonyesha shahidi huyo gazeti la Mawio la Januari 14, 2016 na kumtaka amweleze
Hakimu Simba idadi ya aya za makala inayodaiwa kuwa ya uchochezi iliyokuwa na kichwa
cha habari cha ‘Machafuko yaja Zanzibar’.
Baada ya kuulizwa swali hilo, Kamanda Hamdani alimueleza Lissu kuwa hawezi
kuzihesabu, lakini mahakama ilitoa maelekezo azihesabu, akaomba muda akapewa,
akazihesabu kuwa zipo nane.
Lissu alidai kuwa yeye amezisoma zipo 55 na kwamba aya 37 ni za maneno ya Maalim Seif,
aya nane ni za maneno ya Tundu Lissu, aya nne ni za maneno ya Moyo na kwamba kwenye
aya tatu, ametajwa Rais wa Zanzibar, Dk Ali Mohamed Shein na Kamanda Hamdani alidai
kuwa ni sawa.
Aliendelea kumhoji shahidi huyo wa upande wa mashtaka kwamba:
Lissu: Kwa uelewa wa akili yako anayetajwa mara nyingi kwenye makala hiyo inayodaiwa
kuwa ni ya uchochezi ni nani?
Kamanda Hamdani: Maalim Seif.
Lissu: Wakati unaisoma makala hiyo ulibaini kuwapo kwa matamshi ya chuki na uchochezi
dhidi ya Serikali ni kweli ama si kweli?
Kamanda Hamdani: Ni kweli.
Lissu: Kwa uelewa wako mtu anayetoa matamshi yenye kuibua hamasa au chjuki dhidi ya
Serikali ni lazima uwe uchochezi?
Kamanda Hamdani: Kwa uelewa wangu ni lazima uwe uchochezi.
Lissu: Alimuonesha shahidi huyo hati ya mashtaka na ya maelezo ya awali (PH) na kuuliza
ni sawa nikisema makala nzima ya ‘Machafuko yaja Zanzibar’ ilikuwa ni makala ya
uchochezi?
Kamanda Hamdani: Ni kweli.
Lissu kama makala yote ni ya kichochezi wote walioshiriki ni wachochezi?
Kamanda Hamdani: Ni sahihi.
Lissu: Ni kwa nini Katibu Mkuu wa CUF, Seif Sharif Hamad, Rais Dk Ali Mohamed Shein na
mwanasiasa mkongwe, Hassan Nassor Moyo hawajashtakiwa, kwa nini Tundu Lissu pekee
ameshtakiwa?
Kamanda Hamdani: Jukumu hilo siyo la kwangu, mimi ni mlalamikaji.
Lissu: Kwenye lengo lako mbaya wako alikuwa ni Tundu Lissu?
Kamanda Hamdani: Hapana sina ubaya na Lissu.
Kesi hiyo imeahirishwa hadi Aprili 3, itakapoendelea kusikilizwa.
 
Back
Top Bottom