JembeNaNyundo
JF-Expert Member
- Dec 9, 2016
- 533
- 652
Nimeajiriwa na Serikali miaka 14 na mwezi mmoja sasa. Makato yangu kwenda NSSF hayakuwa yakipelekwa na Serikali hadi mwezi Juni 2016 walipoanza kukata. Nimefuatilia miaka yote hiyo kwa kuandika barua nyingi na kwenda Utumishi, Wizara husika, na pia NSSF lakini hakuna nilichofanikiwa hadi awamu ya Magufuli walipoanza kunikata.
Sasa shida yangu ni moja. Kwa kuwa mimi nilikuwa ninahangaika makato yangu yapelekwe, na kwa kuwa serikali haikunisaidia; sasa Je, naweza iomba serikali ipeleke mchango wake NSSF kwa miaka yote ambayo ilipaswa kuutoa pindi wakati hawajaanza kunikata?