Manyema FC: Hongereni Wacheza! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Manyema FC: Hongereni Wacheza!

Discussion in 'Sports' started by Field Marshall ES, Mar 14, 2009.

 1. Field Marshall ES

  Field Marshall ES JF-Expert Member

  #1
  Mar 14, 2009
  Joined: Apr 27, 2006
  Messages: 12,659
  Likes Received: 67
  Trophy Points: 0


  - Naomba kutoa heshima zangu za dhati sana na za kutoka moyoni kwangu kwa wachezaji wote na viongozi wa timu yetu ya Manyema FC, kutoka Kariakoo kwa kuweza kushinda hivi karibuni na kurudi tena kwenye ligi ya soka ya daraja la kwanza Tanzania.

  - Manyema FC ni timu yangu ya niliyowahi kuichezea miaka ya zamani enzi hizo ikiitwa Stella Maris FC, ikijulikana kama timu ya mabaharia kabla ya kuitwa Muungano Sports, Nanga FC, na hatimaye kuwa Manyema FC mpaka sasa. Ninawakumbuka wale wote niliowahi kushirki nao katika timu hii ikiwa ni pamoja na na Gebo Peter, Imma Peter, Raja Kaka RIP, Juma Jagan, Mlela Mrisho, Idd Pazi "Father", Rashid Hamzuruni, Makobe, Omondi, Jamhuri "Hulio" Kiwelo, Abbasi Senga, Ommi, Patric Rugaimukamu, na wengineo ambao wengi ni marehemu sasa, Mungu awaweke mahali pema na hasa Mkulu Marijani Rajabu aliyekuwa chiriku wa timu.

  - Ninasema nimefurahishwa sana na timu yetu kurudi tena kwenye ligi kuu, sasa ni kazi kwetu wanachama na wapenzi kutoa misaada ya hali na mali, kuweza kuisaidia timu yetu. Ninawaomba viongozi wa timu kina Gebo, Kibadeni "King" na Jamhuri "Hulio" ambao wana elimu kubwa sana ya kandanda kuwapa moyo na elimu hiyo zaidi wachezaji wetu wachanga kimichezo ili waweze kumudu michuano ya ligi na kuweza kuibukia kidedea.

  Mkulu Gebo, kama tulivyoongea jana sisi tutatafuta wafadhili na kuleta jezi na mipira zaidi kwa timu yetu, pia tutajaribu kutafuta michango kutoka kwa wafadhili wakubwa zaidi, na hasa baada ya kupata video rasmi ya wachezaji wetu, tunaomba na wengine ndugu zangu tujiunge tukijisikia kuisaidia timu hii ya vijana wadogo walalahoi wa Kariakoo, katika kuendeleza soka la taifa letu ambalo limeshuka sana. Kwa mwananchi yoyote mwenye kutaka kusaidia timu hii tafadhali tuwasiliane kwenye mtuwameli(at)yahoo.com au kwa JF-PM, mbarikiwe na mtalipwa na Mungu tu.

  Mungu Aibariki Tanzania na Manyema FC.

  Respect - FMES!
   
 2. S

  Sahiba JF-Expert Member

  #2
  Mar 14, 2009
  Joined: Dec 22, 2008
  Messages: 303
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  We umemsahau ally Mmanga.

  SAHYBA
   
 3. Lambardi

  Lambardi JF-Expert Member

  #3
  Mar 14, 2009
  Joined: Feb 7, 2008
  Messages: 10,306
  Likes Received: 5,596
  Trophy Points: 280
  Jamani kurudiligi kuu ni ushindi mzuri sana na mkubwa ila kuweza kubakiahata misimu 3 ndio iwe. Lengo maana angalia wenzenu villa S nawengine kazi inakuwa kupandisha team tukila mwana mnashuka tena.
   
 4. Field Marshall ES

  Field Marshall ES JF-Expert Member

  #4
  Mar 15, 2009
  Joined: Apr 27, 2006
  Messages: 12,659
  Likes Received: 67
  Trophy Points: 0
  - Ni kweli mkuu ni lazima kuwa na plan B, maana A lazima iwe kushinda ubingwa kwanza na B kubaki ligi kuu.

  Hapa wito ni wakulu wote wa nyumbani, jamani shime tusaidie watoto wa nyumbani I mean kina Fresh jumbe mzee wa Jap, Papa Musofe, Papa Msilwa, Ally Rashid, Mkulu Yusuf Kaungu na wakulu wote huko Dubai, Jongo matelefone, Ally Choki, na wengineo simameni mhesabiwe tusaidie timu yetu, msisahau tulikotoka.

  Respect!
   
Loading...