Manunuzi ya Sukari no ya simu,majina na balozi wanahusika

Ngongo

JF-Expert Member
Sep 20, 2008
19,936
34,417
Heshima sana wanajamvi,

Leo asubuhi wakati najiandaa kwenda kibarua nilipewa taarifa na msaidizi (house girl) Sukari imekwisha,nikampatia tsh 10,000/= nikamwagiza atumie yote kwaajili ya manunuzi ya sukari maana bei yake haijulikani.

Baada ya dakika 10 karejea na sukari kilo moja na kunirejeshea ths 8,200/= nikamuuliza kwanini akununua kilo tano akanijubu siku hizi inauzwa kilo moja tu tena unaaandika namba ya simu,jina lako na mtaa unaoishi kama haujulikani vizuri lazima Balozi wa nyumba kumi akutambulishe.

Nimebaki najiuliza nchi inakwenda wapi.

Nawasilisha nikiwa na majozi na msongo mkubwa wa mawazo
 
Mko na bahati huko hata hiyo kg 1 inapatika kwa 1800 tsh..Niko Arusha jana ilinibidi nizunguke mji mzima kutafuta Sukari bila mafanikio nikajikuta nimefika Mirerani nikanunua sukari kilo sh 3800 na ndiyo nikamalizia kg 5 za mwisho..
 
Manuu ngogo ni wa njiro nenda ukanunue huko
 
Nenda Njiro Ghorofa mbili duka la Kiwory utauziwa kilo moja tu lakini lazima useme unaishi Block gani,Balozi wako nani,jirani yako nani kama Balozi humjui,Jirani yako lazima awe maarufu kidogo kama ni mtu wa kujichimbia ndani hajulikani vizuri umekwisha,number ya simu,kitambulisho cha mpiga kura si kile cha zamani kama huna kipya imekula kwako.

Ukitaka kununua kilo moja nyingine ni mpaka week moja ipite kwanza nayo itakuwa maswali yafuatayo.
1. Unatengeza Maandazi.
2. Una watoto wangapi.
3.Unakunywa chai asubuhi tu,kama unakunywa chai na jioni imekula kwako lazima tujibane.
4. Una tabia ya kukaribisha karibisha wageni hovyo kama jibu ni ndio unawapatia kama jibu ni chai imekula kwako.Ni kwanini usiwape maji ya Kilimanjaro yana heshima sana.
 
Kumbafu, watoto watakunywa maji
 
Ngogo is it true? Are you serious?
 
Ngogo is it true? Are you serious?

Mkuu umri wangu umekwenda kidogo mambo ya msingi kama haya siweki utani.Kama uko Arusha leo ukienda duka la Kiwory Njiro utakuta jina langu,namba yangu ya simu na jina la balozi wangu na plot/block nyumba yangu kisa eti ni tsh 1,800/= per kilo.

Sijui madhumuni haswa ya Serekali lakini kilicho wazi wamechemka haswa.
 
Duh! Kama ni hivyo ni hatari! !! Tunarudi miaka ile ya kupanga foleni kununua sukari!
 
Back
Top Bottom