Mansour Himid: Hata nikivuliwa uwanachama wa CCM, sitabadili mawazo yangu kuhusu Muungano

abdulahsaf

JF-Expert Member
Aug 31, 2010
858
130


Na Salma Said,


Mweka Hazina wa Chama cha Mapinduzi kwa upande wa Zanzibar, Mansour Yusuf Himidi, amesema atasimamia mtazamo wake kuhusu muundo wa Muungano wa Tanganyika na Zanzibar unaofaa hata kama itapelekea kuvuliwa uwanachama.

Mwandishi wa DW Zanzibar, Salma Said, amefanya mahojiano na Mansour Yussuf Himidi, ambaye ni waziri katika Serikali ya Mapinduzi Zanzibar na pia Mweka Hazina wa Chama cha Mapinduzi (CCM) kuhusiana na kauli za Katibu Mwenezi wa chama hicho, Nape Nnauye, na wajumbe wa CCM mkoa wa Mjini Magharibi, kumtaka arudishe kadi ikiwa hakubaliani na sera ya sasa ya serikali mbili za Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.


Habari hii kwa kirefu na audio clip, soma post HII



 
Watu kama huyo Yusufu Himid ndo ndumila kuwili, kutumikia mabwana wawili na kujaribu kufaidi kote.
Aondoke katika gari kubwa la CCM kabla ya kutoswa kwa aibu.
Kama hakubliani na ser za CCM si aingie Uamsho tu na aandamane?
 
Huyu Mh kaamua kuwa wazi kuwa mfuasi wa uamsho alie madarakani!heri yake ameonyesha sura ya ukweli kuliko wanafiki wanajificha sura zao kiwiliwili kiko wazi nje ...sasa wanajificha nini??ukweli haujifichi kamwe!
 
kama uamsho wazanzibari sote ni uamsho. mmemsikia Nassor Moyo, waziri wa sheria wa Jamhuri ya mungano wa mwanzo, mama Fatma Karume mke wa muasisi wa dola ya zanzibar, makamo wa CCM zanzibar na Rais mstaafu Karume, mwanasheria mkuu zanzibar, DPP zanzibar, wawakilishi zanzibar na wengineo.

kwa sasa hakuna anaeweza kuzuia nguvu ya wimbi la mabadiliko


wimbo ni mmoja tu kwa sote:

"tunataka nchi yetu sasa tumechoka "
 
Kuna watu wamefilisika kimawazo wanaoeneza upuuzi kuwa kuna watu wanalazimisha na kung'ang'ania Muungano! Ili iweje? Ili tupate nini?!? Its a matter of nguvu ya hoja sio hoja ya nguvu!
UKISIKILIZA VIZURI NILICHOSEMA, UPO UTARATIBU WA KUFIKISHA MAWAZO KWA KIONGOZI WA CCM, SIO KUROPOKA BARABARANI! LAKINI SWALI LANGU KUBWA HAPA....... NANI ANALAZIMISHA MUUNGANO? ILI APATE NINI?NASEMA WANAOSAMBAZA MAWAZO HAYO WAMEFILISIKA KIMAWAZO TENA SANA!
 
Mheshimiwa Nape,
Kwanza kabisa nikusihi usijibu hoja za matusi kama za huyo mtu wa pwani, matusi ni dalili za ukosefu wa hoja kwahiyo achana na wanaotukana, wewe jikite katika hoja zenye mantiki.

Nikirejea katika maswali niliyo nayo, labda nikuulize je ni busara kuandika katiba ya JMT ili hali kuna sintofahamu juu ya hatima ya muungano?

Swali la pili, kwa vile chama chako CCM kipo madarakani kwa zaidi ya miaka 40 kuanzia muungano(TANU/ASP) na hakikuweza kutatua malalmiko ya muungano, unadhani kuna njia gani mbadala itakayotumika kuhimili vishindo vya serikali 2 ikiwa hiyo imeshindikana siku za nyuma?

Tatu, Unadhani ni nini tatizo kubwa linaloutikisa muungano kwa sasa.

Shukran
 
Umenena vyema mkuu, Nnauye Jr, kuna wanaodhani tunalazimisha muungano.

 
Last edited by a moderator:

Ni masuali matatu yaliyotulia,ndani ya maswali hayo ndo sababu iliyomfanya mtu wapwani atukane matusi juu ya nape kwasababu sera ya ccm ni serikali 2 kwenda 1 na matatizo yake yameshaonekana njia za kuondoa hata watoto wadogo wanaelewa cha kushangaza nape na wenzake unapowaelekeza wanakubali juu ya matatizo hayo njia mbadala ipo lakin sera ya ccm ndo inayokandamiza suluhsho hlo.

Hapo inaonesha wazi sera na ilani ya CCM hata kama inamatatizo juu ya utawala nape hawezi kuizungumzia kwasababu yeye ndo msimamiaji wa sera hzo na hapo ndo sababu yakutukanwa kwa nape.swali lakujiuliza,je nikweli nape atakuwa mstar wa mbele na kukubali juu muundo wa serikali tatu?

Na kama atakubali yupo tayar kuikana ilani ya chama chake?kama hayupo tayar juu ya maswali hayo 2 hakuna jema ila ni maneno mabaya juu ya wananchi
 

aongezee na hili.

1. Ni sababu gani zilitumika kuchagua serikali mbili ya tanzania na ya mapinduzi ya zanzibar?
2. Ni kwa nini serikali ya tanganyika iliuwawa kikatili na hivyo kutuondoshea heshima yetu mbele ya mataifa?
3. Iwapo wazanzibar wanulalamikia muungano ili hali wana serikali na wanafaidika mara mbili kwamba wanaweza kuongoza bara na visiwani, Je sisi watanganyika maumivu yetu mliyapima na kujua ni kiasi gani tunaathirika kwa kukosa serikali yetu?
4. Hivi ni sahihi ukoloni mamboleo ukatekelezwa na watu kiduchu wazanzibar, tena wasiotuzidi kwa lolote? iweje watutawale lakini sisi tusiwatawale?
 
Mtazamo wangu kuhusu hilo la Tanganyika kuuawa kinyemela ni kuwa, Aliyekuwa anataka muungano ni Mwl. Nyerere na ili wazanzibar wakubali ikabidi akubali kupoteza taifa lake alilolipigania hadi uhuru.

Hapa ndipo usaliti wa Watanganyika ulipo. Sasa kwakuwa TANU iliwasaliti watanganyika na kuamua ife izaliwe CCM. CCM sasa lazima ilinde usaliti wake wa Watanganyika.

Lamsingi wakubali mjadala na kuheshimu mawazo ya wananchi.
 

mkuu tegemea majibu mepesi kwa maswali mazito.!
 
ZIwe serekali Moja ,Mbili au Kumi si tunachotaka ni sera dhabili za kuendeleza uchumi na siyo blabla tu.Muungano ujadiliwe kwenye ngazi zote ,mapungufu yawekwe sawa yafanyiwe kazi tuendelee na shughuli za maendeleo.Kuna watu wanapinga Muungano lakini cha ajabu ukiwauliza wanapinga hasa nini hana jibu tunakuwa washabiki tu!Mimi sidhani hakuna kitu ambacho hakishughulikiwi ila kinashughulikiwaje!na huwezi kumridhisha kila mtu hata kama chama kingine kitatawala.
 
Kumbe kijana wa changanyikeni umo katika wale wanaotaka serikali tatu. Ila usiwe mkali sana kwa haya madudu mengine humu JF, utapasuka mishipa ya damu bure.
 

Upopo hatari.
 
Namkumbuka Mtikila, "saa ya ukombozi ni sasa" Uzuzu umetuzidi watanganyika. hakuna mjadala hapa. hatukushirikiswa kukolonisha Tanganika kwa Tanzania, Tanganyika ni koloni. Muungano huu wa hovyo ndio unaofanya dhahabu yetu ichimbwe kwa asilimia 3%. Tanganyika itakaporudi, hakika wote walioiba dhahabu na Tanzanaite watalipa.
 

Nyinyi ndio mnaolazimisha Muungano ,nyinyi mnajua fika kuwa Muungano huu ukivunjika basi vyeo vyenu vyote vinaanguka ,Nyinyi mnajua fika kuwa Muungano ukivunjika serikali ya Muungano inapoteza uhalali wa kuwepo,Nyinyi mnajua fika kuwa Muungano ukivunjika mnapoteza haki ya kuwa Chama tawala ,Nyinyi mnajua fika kuwa Muungano ukivunjika uhalali wa Bunge unavunjika ,Nyinyi mnajua kwa undani kabisa Muungano ukivunjika CCM ndio mwisho wake.

Mnaofilisika kimawazo ni ninyi mnaoelekea ukingoni ,Hivi huwajui wanaolazimisha Muungano ? Mbona unajifanya kipofu wewe ,ni akina nani wanaosema wataulinda Muungano kwa njia yeyote ? Pole sana ukisikia kuchamba kwingi.
 
MUUNGANO WA SERIKALI MBILI MWISHO CHUMBE 2015 – WAZANZIBARI

NIMESIKILIZA kwa makini sana maelezo ya Mhe Mansour Yussuf Himid na maelezo ya Nape Mnauye, nikarudia kusikiliza tena kwa mara ya pili ili kuweza kujiridhisha na kufahamu kwa undani hoja za kila mmoja. Hata hivyo, mawazo ya Nape, yamepitwa na wakati.


Kwa ufupi nimegundua kwamba viongozi wa CCM kwa upande wa Bara, yaani Tanganyika bado wanakasumba ile ile ya Nyerere, kutaka kuimeza Zanzibar. Kwa kauli ya Nape, si kweli kuwa Chama chao kina wigo wa kweli wa Demokrasia na uhuru wa kutoa maoni.


Aidha, nimegundua kuwa wanaamini Zanzibar ni mali yao waliyorithi kutoka kwa Nyerere na kusahau wajibu wao wa kuitetea Tanganyika yao na kuimarisha zaidi utawala wa Taifa la Tanganyika, kama wanavyofanya baadhi ya viongozi wa CCM wanaoumizwa na Zanzibar.


Nape, kauli yake iko wazi katika kudai kuendeleza kuitawala Zanzibar, ikibidi hata kwa mabavu na nguvu. Kwa mujibu wa kauli ya Nape, ni wazi kwamba Chama cha CCM, hakina nia njema kwa Zanzibar, kuona ina utawala wenye mamlaka yake kamili.


Nilipokuwa namsikiza nimejiuliza, hivyo kwanini Viongozi wa CCM Tanganyika, wanaumizwa na Zanzibar kuliko Tanganyika yao? Na hapa nimepata picha kwamba hata hizi vurugu na uonevu wa wananchi wa Zanzibar, unasimamiwa na CCM Tanganyika.


Nape Mnauye, anajaribu kuwatisha baadhi ya viongozi wa CCM wa Zanzibar kwa madai ya kupingana na sera za Chama chao. Mansour Yussuf Himid, amesema wazi kuwa sera za CCM si Katiba ya nchi wala si Sheria za nchi ni utaratibu wa Chama tu.


Nakumbuka mwanzoni mwa miaka ya 1980 Julius Nyerere, alisema kuwa Katiba si MSAAFU kwamba haibadiliki. Nape, anashikilia kwamba suala la Muungano kwa sera ya sasa ya CCM ni Serikali mbili.


Mansour, anakubali hilo na wala hakatai, ila anazungumzia mustakabali wa Zanzibar, kufuatana na mabadiliko ya Katiba mpya, hapo baadae. Hapa nimeamini CCM Tanganyika ni mafisadi wa kauli na imani zao.


Nape, anasema mwenye mawazo au maoni wayapeleke katika vikao halali vya CCM, ili yajadiliwe badala ya kuzungumza barabarani. Nape, amesahau kuwa Mansour amekuwa akizungumza kauli hiyo kwa zaidi ya miaka mitatu ndani ya Baraza la Wawakilishi.


Mansour, amezungumza hayo katika mjadala wa rasimu ya Katiba chini ya Samuel Sitta, mwaka jana 2011 na amekuwa akirudia kauli yake ya kukataa Muungano wa Serikali mbili mara kwa mara ndani ya Baraza la Wawakilishi, hadi kudiriki kusema kuwa Muungano huu wa sasa ni BUTU.


Mansour kwa mara ya mwisho nimemsikia tena juzi katika Kongamano lililodhaminiwa na Norway, akisema kuhusu Muungano na muundo wa muungano wenye maslahi kwa Zanzibar. Inashangaza kuwa sehemu zote hizo Nape Mnauye, anaziona ni barabarani.


Nape, anavyo amini sehemu halali iliyotoharika kwa viongozi wa CCM kuzungumzia na kuujadili Muungano ni katika vikao vya CCM tu, wala si mahali pengine. Kumbe jamaa huyu ni mjinga sana na viongozi wote wa CCM Tanganyika wenye mawazo kama ya Nape, nawaweka kapu moja ya wajinga.


Na hapa nazidi kupata picha kwamba matatizo ya muda mrefu kwa Zanzibar, yamekuwa yakichangiwa na Tanganyika, kwa ushirikiano wa baadhi ya Viongozi wachache wa CCM Zanzibar, wanaokubali kuburuzwa na kutawaliwa na Tanganyika.


Kwa taarifa yenu mwaka huu mmeula na chua ‘JINGA LIKIEREVUKA MWEREVU YU MASHAKANI’ ikiwa tuliweza kufikia maamuzi ya kuwa na Serikali ya Umoja wa Kitaifa, naamini na uwezekano wa kuipata Zanzibar yetu, iliyo-huru upo, kupitia viongozi na nguvu ya wananchi wa Zanzibar.


Nape Mnauye, kazi waliyofanya Jumuiya ya Uamsho, ilikuwa kazi ya kigoma cha kuamsha kula daku, ilikuwa ni kazi maalumu waliyopewa na Wazanzibari. Tunakuhakikishia muda si mrefu kwamba Muungano wa Serikali mbili utakuwa mwisho CHUMBE.


WATUACHE TUPUMUWEE..
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…