Manowari za Iran zatia nanga bandari ya Dar, Tanzania

DesertStorm

JF-Expert Member
Nov 22, 2015
3,009
2,416
Machi 01, 2016

Manowari ndogo kadhaa za jeshi la wanamaji la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran zilizobeba ujumbe wa amani na urafiki zimetia nanga katika bandari ya mji mkuu wa Tanzania, Dar es Salaam.

4bk39d2e0c13bb4f8m_620C350.jpg


Akizungumza mbele ya waandishi wa habari katika hafla ya kuzilaki manowari hizo mjini Dar es Salaam leo, balozi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran nchini Tanzania Mehdi Agha Jaafari amesema, lengo la manowari hizo za jeshi la wanamaji la Iran ni kufikisha ujumbe wa amani na urafiki wa wananchi wa Iran kwa watu wa nchi za mashariki mwa Afrika hususan Tanzania.

Amesema kutembelea na kutia nanga manowari za jeshi la majini la Iran katika bandari ya Dar es Salaam ndani ya kipindi cha chini ya miaka miwili kunadhihirisha uhusiano mzuri uliopo baina ya Iran na Tanzania na hamu ya nchi mbili ya kustawisha ushirikiano baina yao katika nyanja za ulinzi.

Manowari ndogo za jeshi la majini la Iran ambazo zinatembelea Tanzania katika utaratibu wa safari ya mafunzo zitakuwepo katika bandari ya Dar es Salaam kwa muda wa siku nne.

Kwa mara ya mwisho, msafara wa manowari ndogo za jeshi la majini la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ulilitia nanga katika bandari hiyo ya mji mkuu wa Tanzania mwezi Juni mwaka 2014...
 

Attachments

  • Screenshot_2016-03-02-13-31-06-1.png
    Screenshot_2016-03-02-13-31-06-1.png
    134.8 KB · Views: 295
  • Screenshot_2016-03-02-13-31-17-1.png
    Screenshot_2016-03-02-13-31-17-1.png
    74.9 KB · Views: 260
  • Screenshot_2016-03-02-13-31-06-1.png
    Screenshot_2016-03-02-13-31-06-1.png
    134.8 KB · Views: 81
  • Screenshot_2016-03-02-13-31-17-1.png
    Screenshot_2016-03-02-13-31-17-1.png
    74.9 KB · Views: 88
Iran ni Washia hawana mahusiano na kundi Lingine zaidi ya Hezbollah na kidogo hamas,,pia nao wamezingatiwa kama makafiri na wenzao..Hawana tatizo maana wana uwezo mkubwa kiakili zaidi ya waarabu.Wana teknolojia nzuri na wanaweza kutusaidia kiteknoloji kama tukitaka na ndiko nyerere alinunua crude bora wakati tukiwa na refinery.
 
You are very wrong.Iran is the most politically independent countries in the world including ofcourse Russia and China.The problem we have is that the big media organizations like the BBC, CNN,Al jazeera and Sky News are controlled by Western countries.These guys hate Iran to the roots because Iran is independent.Many succumb to pressure by western countries even when they should have independent voices and stands.Iran does not.I like Iran.This makes it impossible for them to use Iran and its resources as they would wish and hence the dirty smearing campaign.
Zitakuwa zimekuja kwa mpango maalumu wa Kijeshi...ila hawa jamaa huwa siwaamini kabisa ...nahisi ni ndugu na akina al shabab
 
Ni katika jitihada za kutafuta washilika baada ya kuona mahasimu wao Saudia wanaungwa mkono karibu na kila nchi barani kote, ile ishu ya kufukuzwa mabalozi wao katika nchi nyingi baada ya kifo cha Nimri al nimri imesitusha sana ulimwengu.
 
Eti manowari ndogo,,ha ha ha
hivi kwanini mleta mada anasisitiza sana neno NDOGO.
Atuonyeshe hiyo kubwa basi ikoje hasa
 
jamani mnikosoe kama nimekosea,mm nilijua manowari kiingereza chake ni submarine,
 
Eti manowari ndogo,,ha ha ha
hivi kwanini mleta mada anasisitiza sana neno NDOGO.
Atuonyeshe hiyo kubwa basi ikoje hasa

Hahahaa Elungata si unawajua tena IRAN! Mambo yao ya kisiri mnoo, hebu niambie hiyo manowari wao wanaiita eti NDOGO,, hebu jiulize tu:D..,hawa jamaa hatari sana wanazo kubwa za ajabu,ila hawapendi misifa
 
jamani mnikosoe kama nimekosea,mm nilijua manowari kiingereza chake ni submarine,
submarine kiswahili chake ni nyambizi,niliambiwa neno manowari
ni neo la kiswahili ambalo waswahili walilianzisha kwa kukosea kusoma neno la kiingereza
lililoandikwa "Man of war"
 
Back
Top Bottom