Ndyoko, habari hii umeitoa wapi? Kwa namna ilivyokuwa, je ni sherehe ya kidini(shukrani) au ni sherehe ya kupongezana zaidi na hilo la misa (naamini ameomba kimei kama individual na sio crdb- i stand to be corrected!) labda ni by the way tu kwa sababu wahudhuriaji kwenye sherehe hiyo ya 'kupongezana' walikuwa dar?
Sioni katika hali ya kawaida ni vipi plc kama crdb inaweza kutumia fedha zake kwa ajili ya 'misa ya shukrani'. Hata auditors kwa auditors tu hili haliwrzi kupita kama lilivyo! Utafanya jambo jema kama utaweka/utatafuta maelezo zaidi katika habari hii.
Jamani naombeni msaada hapohapo hivi CRDB ni mali ya umma au?
Udini mbaya....
Hili la misa ya shukrani sijapata kulisikia hata kwa kampuni ndogo ambazo wamiliki ndio hao hao waendeshaji! Nina mashaka hata Mkombozi Bank (plc?) kama wameshawahi kufanya misa ya namna hii. Well, ngoja tusubiri..yawezekana ni 'maendeleo' katika corporate governance!SMU,
Hata mimi nafikiri kama wewe. Haiingii akilini CEO wa PLC atumie fedha za benki kwa shughuli ya kikanisa.
Hapa kuna possibilities mbili.
1. Kuna smear campaign na habari hizi hazina ukweli.
2. Bongo imeoza kiasi kwamba mambo ya kweli yakianikwa yanaonekana kama smear campaign.
I hope it is the first one, because if it is the second one, tupo pabaya kuliko nilivyofikiri.
Sawa hajalazimishwa mtu kuhudhuria.
Lakini kwa nini anatumia fedha za benki, benki isiyo na dini, benki yenye wateja wa dini zote na wengine wasio na dini, benki ya umma katika nchi isiyofuata dini yoyote, kufanikisha misa ya dini moja?
Wafanyakazi wa dini nyingine wakisema wamebaguliwa kwa sababu hawajafanya yao atakubali kwamba kawabagua?
Tunaoamini kwamba kutumia fedha za shirika la umma katika shughuli za kidini tukisema amekosea atakataa?
Kufuatana na sheria za mabenki yote, CEO hawezi kujiamulia yeye mwenyewe kutumia fedha kwa njia yeyote ile bila kupata idhini ya bodi yake! Yote mnayosema kuwa Kimei wa CRDB ameyafanya kama ni kweli basi bodi yake imeidhinisha ama sivyo kama bodi ya CRDB haikiudhinisha matumizi hayo ,anaweza kuchukuliwa disciplinary action.
Wewe ndio mbumbumbu wa mwisho! changia hoja, nachojua sio kila mfanyakazi CRDB ni mkristio! ambacho angefanya nikumshukuru mungu kwa kuita viongozi wote wa dini na kuomba au kushukuru!!
Siku nyingine think!
hiyo faida wanayopata wawakumbuke wateja,watupe mikopo ya riba nafuu.
Tatizo lako na wengine wote wenye mitazamo kama ya kwako ni tabia yenu ya ushindani wa kitoto, unajua watoto wana tabia ya kulilia kila anachopewa mtoto mwenzake.
Mkuu wa benki ni mkiristo ameamua kwenda kanisani kuhurudhisha mafanikio ya kazi yake kwa Mungu wake na kutoa shukrani, sasa wewe unataka eti amshirikishe na mungu mwingine nje na imani yake. Mkuu wa bank hakuwa mchoyo badala ya kwenda peke yake kutoa shukrani na kujizolea mibaraka lukuki peke yake yeye amewapa nafasi wafanyakazi wengine pia, wale waliojisikia huru kuandamana nae.
Unajua mwisho wa mwaka makampuni mengi hufanya sherehe za kumaliza mwaka, ukubwa wa sherehe unategemea na uwezo wa kampuni, hapa CRDB wameweza kukutanisha wafanyakazi wao wa kutoka maeneo mbalimbali jambo ambalo ni jema kwa kampuni. Kwenda kanisani ni suala binafsi la mkuu wa benki na wale wafanyakazi walioafiki kumuunga mkono, hili ni tukio moja tu kati ya matukio mengi na mbwembwe zao za kusherekea mwisho wa mwaka.
Mwandishi hapa ama kwa maslahi yake binafsi au kwa kutokuelewa anataka atuamishe kuwa sherehe nzima ilikuwa ni misa kanisani tu.
Hakuna ubaya kwa viongozi kwenda kuabudu hata rais wa nchi pia anahudhuria nyumba za ibada huku akiwa madarakani huku akijua kabisa kuwa yeye ni rais wa watu wa dini zote na wasio na dini pia. Tena apokwenda kuabudu anasindikizwa na kulindwa na vyombo vya dola, kwa nini hatulalamikii utumiaji wa raslimali za serkali na rais anapokwenda kuabudu mskitini au kanisani? kwa nini asiite viongozi wa dini zote na kuomba au kushukuru huko huko ikulu?
public limited company.naomba maana ya hili neno PLC?