Manji huenda sio raia wa Tanzania

Rafa kilenza

Member
Jan 23, 2017
32
30
Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inakataza mtanzania yeyote yule kumiliki
uraia wa nchi mbili

Ni kosa kubwa kisheria kumiliki Hati za kusafiria(Passport) za nchi mbili tofauti
Mtanzania yeyote yule anayemiliki uraia wa nchi mbili huyo ametenda kosa la Jinai

Kama ni kweli Yusufu Manji anamiliki passport za nchi mbili tofauti hilo ni kosa kubwa sana na haitajiki kuwe na siasa katika hili

Anapaswa kulipa kodi zote kama mwekezaji wa nje na sio wa ndani kuanzia siku ya kwanza anaanza biashara hapa nchini
Anapaswa kufukuzwa nchini mara moja kwa kutenda kosa hilo

Raia wa kigeni hana haki ya kumiliki ardhi ndani ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa mujibu wa sheria ya ardhi ya mwaka 1999
Kwa hali hiyo ardhi yote anayomiliki Manji inapaswa kurudishwa serikalini mara moja na hatua za kisheria zifuatwe
Na yeyote yule aliyehusika katika kudanganya adi kumsaidia huyu mtu kupata hati ya kusafiria ya Tanzania anapaswa kuwajibika maana huu ni uzembe wa hali ya juu

Hii nchi ni yetu sote na ni lazima sasa utawala wa sheria ufuatwe
Tumuunge mkono Rais JPM katika mambo kama haya maana tulishazoea kuishi kwa mozoea

Rafa lukindo
0765499321
 
Kuna tetesi kuwa Yusuph Manji huenda sio raia wa Tanzania. Wengi wanashangaa kwanini asiwe raia wakati kazaliwa Tanzania?

Yeyote mwenye swali kuhusu uraia/uraia pacha na uwezekano wa Manji kuwa sio raia wakati kazaliwa Tz anakaribishwa apate elimu ya uraia hapa karibu.
 
Back
Top Bottom