ras mkweli
JF-Expert Member
- Mar 12, 2012
- 280
- 104
Hakimu Mfawidhi, Cyprian Mkeha ameiahirisha kesi hiyo mara baada ya Wakili wa Serikali, Adolf Mkinii kudai upelelezi bado haujakamilika.
Manji alikuwepo Mahakamani leo kwani mara ya mwisho aliagizwa awe anafika.
Manji alifikishwa mahakamani hapo kwa mara ya kwanza Februari 16, 2017 ambapo anadaiwa kuwa, kati ya Februari 6 na 9, 2017 katika eneo la Upanga Sea View Ilala alitumia dawa za kulevya aina ya Heroin.
Chanzo: Mwananchi