Manji ameipa klabu ya Yanga SC hekari 715 Geza Ulole

Mr Hero

JF-Expert Member
Jun 11, 2015
5,542
7,450
MWENYEKITI wa Yanga SC, Yussuf Mehboob Manji ameipa klabu hiyo eneo la ekari 715 lilipo Geza Ulole, Kigamboni, Dar es Salaam.Wasaidizi wa Manji wamekabidhi eneo hilo leo mchana katika hafla fupi iliyohudhuriwa na Waziri wa Mambo ya Ndani, Mwigulu Nchemba na Maofisa wa chama na Serikali ya Kigamboni.

Aliyepokea eneo hilo kwa niaba ya klabu ni Mwenyekiti wa Baraza la Wadhamini wa klabu, Mama Fatma Karume aliyeambatana na Mjumbe mwingine wa Bodi hiyo, Dk. Jabir Idris Katundu, Mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya klabu, Samuel Lukumay na Katibu Mkuu, Baraka Deusdedit.

Sasa rasmi utafanyika ujenzi wa uwanja na uwekezaji mwingine katika eneo hilo lililobatizwa kijiji cha Yanga SC.
 
Amewapa na documents ie title deeds? Wamesaini mkataba wa kuhamisha umuliki? Au wameoneshwa mipaka tu wakaambiwa kuanzia leo ni mali yenu?
 
Maji anajificha kwenye kichaka cha karanga, subr j2 matokeo yawe kinyume ndipo atakapo wajua yanga kuwa amewapiga nusu kaputi au lah
Yangu macho....
Roho yako hapo ilipo inatamani ipasuke jinsi ulivyoijaza chuki
 
Hii ndio yanga,vitendo tu,na nimesikia kila goal j mosi analinunua sh mil 5 hahahaha hebu igeni na nyie.
 
14516616_330249287323003_1443382279390666658_n.jpg
 
Hahaha! Jangwani city basi tena!anyway kama ni kweli sasa tunaanza kuona hatua za dhati na dhabiti kuikwamua Yanga,Lakini Ile habari ya jangwani city ilikuwa changa la macho ..!mabasi ya mwendo kasi yakae wapi?
 
Amewapa na documents ie title deeds? Wamesaini mkataba wa kuhamisha umuliki? Au wameoneshwa mipaka tu wakaambiwa kuanzia leo ni mali yenu?
Kampuni ya Yanga yetu ambayo inawania nafasi ya kuikodi Yanga kwa miaka 10 imekabidhi hati kabla ya kuanza ujenzi wa mazoezi wa kikosi cha Yanga.
Uwanja huo wa Yanga uko katika eneo la Gezaulole jijini Dar es Salaam na Waziri wa Mambo ya Ndani, Mwigulu Nchemba alikuwepo katika hafla hiyo fupi.
Wakati Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini wa Yanga, Mama Karume pia alikuwa kati ya waliohudhuria shughuli hiyo.
Ujenzi utakapokamilika, Yanga itakuwa na uwanja wake wa mazoezi ambao unatarajia kuwekewa nyasi bandia.
 
MWENYEKITI wa Yanga SC, Yussuf Mehboob Manji ameipa klabu hiyo eneo la ekari 715 lilipo Geza Ulole, Kigamboni, Dar es Salaam.Wasaidizi wa Manji wamekabidhi eneo hilo leo mchana katika hafla fupi iliyohudhuriwa na Waziri wa Mambo ya Ndani, Mwigulu Nchemba na Maofisa wa chama na Serikali ya Kigamboni.

Aliyepokea eneo hilo kwa niaba ya klabu ni Mwenyekiti wa Baraza la Wadhamini wa klabu, Mama Fatma Karume aliyeambatana na Mjumbe mwingine wa Bodi hiyo, Dk. Jabir Idris Katundu, Mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya klabu, Samuel Lukumay na Katibu Mkuu, Baraka Deusdedit.

Sasa rasmi utafanyika ujenzi wa uwanja na uwekezaji mwingine katika eneo hilo lililobatizwa kijiji cha Yanga SC.
 
Hii si habari njema kwa MIKIA FC,watajua tofauti ya wakimataifa na wamatopeni ila nashauri tuache siasa ktk hili wana yanga tuwe pamoja tuweke itikadi pembeni ili YANGA IWE DAIMA MBELEEEE
 
Najua huyu Mhindi anaandika kila kitu afu wakianza Kuleta wenge baadae awaonyeshe karatasi wampe chake aachie timu lakini ngoja J1 Tumfunge mpaka abadilike sura kuwa mweusi..
 
Back
Top Bottom