Manispaa ya Songea kushamiri upinzani

Ne Mbwitu

JF-Expert Member
Aug 23, 2020
275
802
Baadhi ya kata katika manispaa hii ni wazi zitaangukia mikononi mwa vyama vya upinzani vya CHADEMA na ACT. Hii ni kutokana na wagombea waliopitishwa na CCM kukithiri kwa vitendo vya rushwa.

Tetesi zinasema kuwa wagombea hawa hawapendwi na wanachama na wananchi ila wanabebwa na viongozi wa wilaya na mkoa. Hivyo, wanachama wa CCM (wajumbe na wasio wajumbe) na wananchi wa kata hizi wameamua kuungana na kuja na kauli mbiu kuwa safari hii wanachagua mtu sio chama.

Kwa umoja huu wa wanachama na wananchi ni dhahiri tutaiona manispaa ikiwa na sura za madiwani kutokea upinzani. Pia umoja huu utahatarisha harakati za Ndumbaro za kusaka kura za ubunge kwani upinzani wamesimamisha wagombea machachari katika nafasi ya ubunge.

Maendeleo hayana chama
 
Watatangazwa vizuri tu,huyu anayeongoza kuwatangaza basi atakuwa hataki kuishi .

Watu wamechoka na kila kitu cha hii awamu

Kauli hii ndio Babati anahitaji kusikia anajipa matumaini kuwa NYANDA YA KASKAZINI ina akili kubwa mpaka imewakamata mazwazwa ya KUSINI.
 
Back
Top Bottom