Manispaa ya Moshi: Soko la Mbuyuni uchafu umezidi

Manispaa ya Moshi: Soko la Mbuyuni uchafu umezidi

NIFEDIPINE

JF-Expert Member
Joined
Aug 16, 2013
Posts
216
Reaction score
225
Naandika kwa kukerwa sana na watu wasiojitambua wenye wajibu wa kuhakikisha wanaweka manispaa katika hali ya usafi kutotimiza wajibu wao.

Wengi tunafahamu kuwa kilimanjaro ni mkoa unaoongoza kwa usafi na mara kwa mara umekuwa ukichukua kombe la kuwa mkoa msafi Tanzania.

Tangu mwisho wa mwaka 2017 mpaka sasa kumekuwa na hali ya kutojali kutoka katika manispaa ya moshi hasa kwa watu waliopewa dhamana ya kuweka manispaa safi KUACHA takataka kujaa katika soko la mbuyuni hasa pale ambapo magari ya weruweru yanapopaki kusubiria abiria.

Kusema ukweli TAKATAKA ZIMEJAA mpaka zinakaribia kuziba barabara ya LAMI kiasi kwamba magari hayawezi kupishana kwenye barabara hii.

Naomba wahusika wenye dhamana wahakikishe uchafu huo uliorundikana barabarani unatolewa haraka iwezekanavyo.

Gari la takataka la manispaa lipo,kwahiyo sioni sababu kwanini wanashindwa kutoa huo uchafu uliotapakaa BARABARANI.

Msisubiri mkuubwa mkoa apite au mkuu wa wilaya apite na kuwatumbua kwa kutokuwajibika kwenu kwa makusudi.

Mliomba kazi. Msione kazi kufanya kazi.

Nawasilisha
 
wamejitaidi kukusanya apo wazoaji wanazuga kama hawajaona
 
Back
Top Bottom