Baada ya Serikali ya awamu ya 5 kuingia madarakani ilifanya mabadiliko mengi yakiwemo baadhi ya makusanyo yawekwe Benki Kuu, nyingine zilifutwa... (tozo, ushuru, ada, kodi nk) Manispaa zilipaza sauti kuondolewa kwa sehemu ya Mapato.
Lakini mbona huko mitaani kuna Vyanzo ambavyo havijawahi kuongelewa? mfano mkoa wa Kilimanjaro Pick up zote zinazobeba mizigo zimepewa namba ubavuni Taxi... hapo ujue hizo namba nichanzo cha Mapato, mikokoteni yote inabeba mzigo ndani ya Manispaa nayo inayo namba za ubavuni...
Nashauri kwa Jiji kama D' salaam kama wataamua Pick up zote Maarufu kama Virikuu kama zingepewa namba za ubavuni kingekuwa chanzo cha Mapato... Baraza zote zinazouza Chips usiku kama zingekuwa zimesajiliwa kwa Bwana Afya wa Manispaa pia kingekuwa chanzo cha Mapato.. Kama walikuwa wanamtoza ushuru wa Soko mwenye kufanyabiashara barabarani kwa kisingizio yupo maeneo ya Soko kwanini hawalioni hili?
Sehemu zote wanazouza Juice ya miwa kama wangesajiliwa kwa Bwana Afya pia kingekuwa chanzo cha Mapato.