'Manispaa Kinondoni itaje vigezo kugawa majimbo'


S

Serayamajimbo

Senior Member
Joined
Apr 15, 2009
Messages
191
Likes
0
Points
0
S

Serayamajimbo

Senior Member
Joined Apr 15, 2009
191 0 0
na Betty Kangonga


amka2.gif

CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kupitia sekretariati yake imeitaka Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni kuweka hadharani vigezo vilivyotumika kutoa mapendekezo ya kugawa majimbo.
Taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari jana na katibu wa chama hicho jimbo la Ubungo, Nasor Balozi, ilieleza kutokana na taarifa ya Februari 11 mwaka huu iliyotaja tarehe ya mwisho ya kupeleka maoni kwenye kata haitoshi wadau kujadiliana na kuomba kusogeza mbele tarehe hizo.
Kupitia tamko hilo wameshauri halmashauri hiyo kuitisha haraka mkutano wa wadau vikiwemo vyama vya siasa, ili kujadiliana mapendekezo hayo mapema iwezekanavyo.
“Tunamtaka mkurugenzi na uongozi wa manispaa kama maelekezo yaliyotolewa na Tume ya Uchaguzi katika mkutano wake na vyama hivyo ngazi ya taifa wa tarehe 20 Januari mwaka huu kwamba mchakato wa kuleta maombi unapaswa kuhusisha mapendekezo na wadau kushirikishwa kwa ukaribu zaidi,” ilieleza taarifa hiyo.
Iliendelea manispaa inapaswa kwanza ingeanza mchakato wa ugawanyaji wa kata kabla ya kujadili kuhusu mgawo wa majimbo; hii ni kwa sababu majimbo yanaundwa na kata na tayari kuna maelezo yanatolewa kwamba zipo kata ambazo zitagawanywa zikiwemo Kibamba na Kimara katika jimbo la Ubungo na Kawe na Tegeta katika jimbo la Kawe.
Pamoja na hayo chama hicho kilihoji sababu ya kuiondoa kata ya Goba ambayo sasa iko kwenye jimbo la Ubungo na kueleza kusudio la kuipeleka kwenye kundi moja na kata ambazo sasa ziko upande wa jimbo la Kawe (Bunju). Hata hivyo ilipendekezwa kuwa kata za Kimara, Makuburi, Mbezi na Kibamba kuwa katika jimbo la Kibamba; kata hizi kwa sasa ziko katika jimbo la Ubungo.
 

Forum statistics

Threads 1,236,244
Members 475,030
Posts 29,251,507