Katika kile ninachoweza kukiita ni uozo serikalini, nimekutana na uozo huu wa kuendelea kutafunwa kwa pesa za walipa kodi kwenye gazeti la Mwanahalisi Online.
Kila sehemu wizi wizi tuu, lakini bila shaka mwisho wao umefika!
Valentino Mlowola, Mkurugenzi wa Taasisi ya Kuzuia na KUpambana na Rushwa (Takukuru)
MANISPAA ya Ilala jijini Dar es Salaam imetafuna jumla ya Sh. 16 Milioni kutoka kwenye miradi mbalimbali, anaandika Faki Sosi.
Edson Makallo, Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) Mkoa wa Ilala amesema, pesa hizo zililenga kuingizwa kwenye Mfuko wa Dawa ‘Basket Fund.’
Makallo amesema ubadhirifu umefanywa na maofisa kwenye manispaa hiyo na kwamba, hatua za kisheria zitachukuliwa.
Hata hivyo amesema, Takukuru imefanikiwa kuokoa zaidi ya Sh. 104 milioni. Kati ya fedha hizo, Sh. 12 Mil zilidaiwa kuwa malipo ya malimbikozo ya mishahara ya walimu wa Shule za Msingi na Sh. 92 Milioni zilizodaiwa kutengwa kwa ajili ya ujenzi wa barabara ya St Mary’s, Tabata.
Amesema, barabara hiyo ilijengwa chini ya kiwango na kwamba, baada ya uchunguzi mkandarasi alirudisha fedha hizo na yeye (mkandarasi) kuingia hasara.
Ametaja maeneo yanayolalamikiwa na wananchi kwenye manispaa hiyo kuwa serikali za mitaa, mahakama, elimu, mawasiliano (Ttcl na Posta), polisi, maliasili, afya, taasisi za kifedha, Viwanada na Biashara, Mamlaka ya Viwanja vya Ndege, Uhamiaji, Sekta binafsi na Chuo cha Ubaharia.
Chanzo: Mwanahalisi Online