Manispaa DSM mmeshindwa usafi???

chakutaka

Senior Member
Feb 6, 2015
150
14
katika pitapita yangu jijini Dar es Salaam nimeshuhudia uchafu ukizagaa mbele ya nyumba za makazi ama sehemu za bishara. hapa ninachouliza ni kuwa hivi Manispaa mmeshindwa hata kujiwekea vijsheria vidogovidogo vya kuwabana watu wachafu??? kwa nini msiwakamate watu ambao mbele ya maduka yao ni kuchafu na kama eneo linalomzunguka machinga ni chafu kwa nini asipigwe faini?? Baada ya desemba 9 na nyie mmerudi kulala, shame on you.
 
Tatizo la dar ni magari ya manispaa kushindwa kuzoa talka hata kama watu wakijitolea kufanya usafi. Aliyepewa tenda ya kuzoa taka amedhihirisha kushindwa kuzoa taka kwa kiwango kikubwa.
 
Jiji bado lipo chini ya CCM kwa hiyo usishangae ndugu! Subiri wawape wenyewe Ukawa utaona MABADILIKO !
 
Vipi mfunga viatu ameshindwa kazi,aje kwangu awe ananifulia ,
 
Tunangoja Magufuli atoe amri ndio tuwajibike,hadi mkuu wa mkoa nae anasubiria amri.
 
Alafu ukifuatilia manispaa utakuta kuna mzabuni ana tenda ya kukusanya taka na anakusanya michango ya kuzoa taka kama kawaida chini ya vitisho vya wagambo wa jiji....
 
Alafu ukifuatilia manispaa utakuta kuna mzabuni ana tenda ya kukusanya taka na anakusanya michango ya kuzoa taka kama kawaida chini ya vitisho vya wagambo wa jiji....
Mara nyingi watu wanalalamika kuwa wanatoa michango ya uzoaji taka lakini taka hazizolewi.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom