Mangula alishukia genge la Lowassa lililomwaga rushwa Zanzibar, Hatua kali kuchukuliwa

Makamu mwenyekiti wa CCM Philip Mangula amesema genge lote lililoshiriki kugawa rushwa Unguja na Pemba kwa wajumbe wa NEC na mkutano mkuu wa CCM hatua kali za kimaadili zinachukuliwa.
"CCM haitamshindwa mtu mmoja anayekivuruga chama..."alisema Mangula.

Wakati huo huo askofu mkuu wa Kanisa KATOLIKI Muadhama Dr Policarp Pengo amewaasa watanzania kutochagua wanaomwaga mabilioni kusaka urais.
attachment.php


mm naona Lowasa wanamuonea mzee wa watu kama alivyosema Sumaye, kwani ni mgombea yupi ndani ya CCM, ambaye hagawi rushwa kwa wananchi na makada wa chama hicho ili aungwe mkono kwenye kinyang'anyiro cha urais, ubunge, udiwani, mwenyekiti na ujumbe wa Serikali za mtaa. Tunazo taarifa wengine waliuza hadi mashamba na mali zao kadhaa ili kutoa rushwa kwa wanachama na wananchi ili wawachague. Ni mgombea yupi ndani ya chama chake aliyepitishwa bila kutoa rushwa,atutajie hata 100 tu, hili nalo ni tatizo.kwa taarifa yako mhe. Mangula wagombea wote sio wasafi na haya wanayafanya kwa staili na namna mbalimbali, wengine wanagawa vitalu, wengine wanatoa misaada ambayo hapo awali hawakuwahi kuitoa, wengine wanaendesha harambee za kujenga makanisa/misikiti n.k. je hawa hatuwaoni, mbona hatua stahiki hatuchukui. hili lilipaswa lifanyike kwa vyama vyote vya siasa chini ya usimamizi wa serikali ni ya ccm. maana rais mtoa na mpokea rushwa akiingia ikulu haijalishi atatoka chama gani wananchi wote akiwemo mhe. mangula tutapata madhara ya rushwa hiyo

ushauri wangu kwa Mangula, aache kuwatishia wagombea, ashughulikie mzizi wa tatizo la rushwa ndani ya chama chake kwasababu haya ya nje ni matokeo tu(majani), mzizi yeye anaujua huo ndio anapaswa kuung'oa haraka ili kurudisha matumaini ya wananchi kwa chama chetu pendwa. itakuwa ni aibu chama hiki kikifia mikononi mwake wakati yeye ni mtalaam aliyebobea katika masuala ya siasa na ana elimu ya kutosha katika eneo hilo.

Ni aibu kwa CCM kulalamikia watu wake kwa rushwa wakati wana jeshi, usalama wa taifa, takukuru, polisi, magereza n.k. Wao kama kweli wanachukizwa na rushwa watumie vyombo hivi wavipe uhuru viwakamate wahusika na kuwafunga kisheria, ndipo rushwa itaisha lakini kama nao wanalalamikia rushwa kama chama cha upinzani wanatukosea heshima watanzania wote tuliowapa ridhaa ya kutuongoza

Mhe.Mangula kumbuka kamati zenu za maadili hazina uwezo wa kumrekebisha mtu na hakuna mwana ccm anayeogopa hizo kamati kwani hata hao wanaweza kuwahonga na watashindwa kutoa maamuzi sahihi. mm niwaulize ccm wenzangu mara ngapi tumewaita watu katika kamati zetu, tukawachukulia hatua na watu wakaacha kufanya waliyokuwa wanafanya?nipatiwe mifano ya watu 10 tu wagombea ngazi za juu.

ccm na uongozi wenu muache kulalamika chukueni hatua kuokoa taifa hili maana matumaini ya wananchi yanakaribia kupotea kutokana na wao pia kutakiwa kutoa rushwa ndipo wahudumiwe katika Ofisi nyingi za nchi hii. hizi ndizo kero zinazowatisha wananchi na kuona kama nchi yao imeuzwa na wao wamebaki kuwa watumwa katika nchi yao. matokeo yake, wananchi wakifikia hapo, wanaweza kufanya maamuzi ambayo sio sahihi wala sio salama kisheria kama kuchoma ofisi za umma na kura za wagombea matukio ya kwenye uchaguzi wa Serikali za mitaa? je ni sahihi haya kutokea


ni ushauri tu ambao mkiutekeleza utawasaidia kuokoa chama chetu pendwa

tukumbuke wosia wa Babab wa Taifa Hayati Mhe. J.K. Nyerere alisema tukikosea tujisahihishe na tujirekebishe

Mhe. Mangula, mie nakutakia mafanikio katika kushughulikia kero za wananchi tuliowapa ridhaa kutuongoza.
 
Mimi ni Mkatoliki lakini napenda kukiri hatuna Mkatoliki anayetosha kumrithi Jakaya.....

Tuache siasa za usisi na sasa tuangalie wa Tz wanamtaka nani?

Hii propaganda ya kumwagia kila dhambi mtu mmoja ni janga kwa umma wetu.
 
Back
Top Bottom