jf user
JF-Expert Member
- Aug 22, 2018
- 777
- 625
Tukisoma historia ya mkoa wa Kilimanjaro tunaona kuna kabila maarufu sana la wachaga ambalo kimsingi lilikua na tawala mbali mbali za kichaga kila chifu na eneo lake.
Machifu hao waliitwa mangi.
Mangi maarufu ni mangi rindi na mamngi meli wa old moshi, mangi sina wa rombo, mangi horombo wa keni. Mangi sina na mangi horombo walisifika sana kivita kwa kujenga jeshi imara.
Mangi sina aliivamia kibosh na kupora mali zao kama ardhi, ngombe na chakula.
Pia kuna mangi mariale wa marangu na mangi petro mariale wa kilema.
Mwaka 1952 ulifanyika uchaguzi ambapo mangi Thomas mariale wa marangu alishinda uchaguzi na kuwa mangi mkuu/president wa mkoa wa Kilimanjaro ambapo aliwawakilisha mangi wengine wa mkoa huo (Mangi wa hai abidieli shingeli, mangi john maruma wa rombo, mangi petro na kilema ambae alijitoa kwenye uchaguzi huo)
Kimsingi kila mangi alilinda utawala wa eneo lake na ndivyo ilivo mpaka sasa wachaga wengi hujenga kwao, hupambana huku na huko na kupeleka faida kwao/uchagani.
Shule za kibinafsi zilianza kujengwa Enzi hizo na ndio maana mkoa wa Kilimanjaro una shule nyingi sana leo hii.
Kwa namna hii mangi wanajulikana kama mabepari wa kwanza wa kijadi.
Wajerumani walipotua mara ya kwanza Kilimanjaro walitua old moshi kwa mangi rindi na huyo ndie aliemsaliti mangi sina ambapo vita vilipiiganwa lakini mangi rindi alikuja kufariki mwaka 1891 hivyo kumwachia kiti mtoto wake mdogo maarufu kama mangi meli.
Wajerumani walikua close sana na mangi Thomas marialle ambapo vita vingine vilitokea na kusababisha mangi meli kuuwawa na kichwa chake kuchukuliwa ujerumani na kipo huko hadi hii leo. Alizikwa kiwiliwili, mti alilonyongwa upo hadi leo huko kibosho.
Familia za machifu zilikua juu kisiasa na watoto wa machifu walisomeshwa ulaya kwaajili ya kuunda serikali ya kwanza ya kikoloni.
Wachaga dio watu wa mwanzo kuupokea ukristo.
Wakati wa harakati za uhuru tawala za kijadi zilianza kukosa nguvu baada ya Thomas mariale kumuunga mkono Nyerere na harakati za TANU za kupata uhuru na bada ya kupatika uhuru tawala zote za kijadi zilifutwa.
Nguvu a Thomas mariale ilianza kupotea Kilimanjaro baada ya kupambana kitaifa na kwa mkoa wake pia alitofauutiana na mangi abdieli wa hai hali iliyomfanya aachie umangi na kumpa ndugu yake kitu kinachotafsiriwa kama mbinu ya kiusalama dhidi ya mangi mkuu Thomas mariale.