Maneno ya Mhe. Zitto, Mhe Ndugai tunahitaji uthibitisho

FAHAD KING

JF-Expert Member
Joined
Sep 14, 2017
Posts
301
Reaction score
377
Mbunge wa kigoma mjini Mh.ZUBERI KABWE aliitwa kwenye mahojiano na kamati ya maadili ya bunge kutokana na kauli yake wanaodai ni ya kichochezi "bunge sikuhizi ni idara ya tawi la utawala".ZITTO alifafanua kwa kutoa thibitisho 10 nayo ni kama zifuatazo...

1. Kuzuiwa kwa "Bunge Live" kwa kisingizio cha kupunguza gharama za uendeshaji wa mhimili wa Bunge, wakati Mikutano yote ya mhimili wa Serikali, hasa ya Rais ikirushwa live (mubashara) ni dalili ya wazi ya kufifisha sauti ya Bunge na kupandisha sauti ya serikali. Hata vituo binafsi ambavyo vilipanga kurusha bunge Live bila malipo (na hivyo kutokuwa na gharama) vilizuiwa, lakini vinarusha Live mikutano ya Rais.

2. Kitendo cha Uongozi wa Bunge kurudisha serikalini shilingi Bilioni 6 bila ridhaa ya wabunge kwa kisingizio kwamba zimebaki kutokana na kubana matumizi. Hii ni dalili ya wazi ya Bunge "kujipendekeza" kwa serikali. Wakati Uongozi wa Bunge ukirejesha kiwango hicho cha Fedha, kuna taarifa kwamba kamati nyingi za Bunge zinashindwa kutekeleza wajibu wake kwa sababu ya ukata.

3. Maelekezo ya mhimili wa Serikali kwa mhimili wa Bunge, kupitia maagizo ya Rais Magufuli kwa Spika Ndugai kuwa "Awashughulikie wabunge" (kwa kuwafukuza bungeni) aliowaita "waropokaji" ili waje wazungumze nje ya Bunge na yeye Rais (Serikali) apate nafasi ya kuwashughulikia. Kauli hii ya Rais aliyoitoa wakati akipokea Ripoti ya Prof. Osoro kuhusu Mikataba ya Madini, Juni 12, 2017 inaonyesha picha iliyo dhahiri kuwa Bunge linapokea Maelekezo kutoka Serikalini ya kuwadhibiti wabunge hasa wanaoiwajibisha serikali. Na hatuwahi kuliona Bunge likiyakana maelekezo hayo ya Rais kwa Spika.

4. Kitendo cha Bunge kuhariri hotuba za kambi ya upinzani kwa kushinikiza kuondolewa kwa vipengele vinavyoikosoa Serikali. Mathalani, Wakati wa Bunge la Bajeti, hotuba ya Msemaji wa Kambi ya upinzani wa Wizara ya Mambo ya Ndani, ndugu Godbless Lema, iliamriwa kuondolewa maneno yanayohusu kashfa ya Mkataba wa Lugumi, kumhusisha Rais na kuuzwa kwa nyumba za Serikali, Mauaji ya wanasiasa, pamoja na Bunge kulinda wahalifu.

5. Kauli ya Rais Magufuli ya Novemba 4, 2016 akizungumza na wahariri wa vyombo vya habari kuwa "mzizi wa mhimili wa serikali ni mrefu zaidi kuliko mihimili mingine" mara baada ya kuulizwa juu ya matumizi ya Serikali Nje ya Bajeti iliyoidhinishwa na bunge, unaonyesha dhahiri fikra ya Rais na Serikali yake juu ya ukuu wa mhimili wa Serikali dhidi ya Bunge.

6. Kitendo cha Ripoti ya Kamati ya Bunge ya Tanzanite na Almasi kusomwa nje ya Bunge na kuwasilishwa kwa Waziri Mkuu na Rais bila kuwasilishwa na kujadiliwa Bungeni ili kuwekewa azimio la Bunge. Kitendo hiki kinaifanya Kamati hiyo kuonekana kuwa ya Serikali badala ya Kamati ya Bunge.

7. Kauli ya Rais kuwa Spika alimpigia simu kumuuliza juu wajumbe wa kuwaweka kwenye Kamati za Bunge za Tanzanite na Almasi inaonyesha dhahiri kuwa Spika anafanya kazi kwa maelekezo ya Rais. Na Bunge na Spika hawajawahi kuikana kauli hii ya Rais.

8. Kwa mara ya kwanza kwenye Historia ya Nchi yetu tumeshuhudia Mbunge akishambuliwa kwa risasi wakati Mkutano wa Bunge ukiwa unaendelea. Haijapata kutokea katika historia ya Bunge letu, Wabunge kukamatwa hovyo mbele ya mageti ya Bunge na kusafirishwa usiku usiku bila hata Spika kujulishwa kama taratibu za Mabunge ya Jumuiya ya Madola zinavyotaka. Kitendo cha 'Watu Wasiojulikana' kummiminia risasi zaidi ya thelathini Mbunge wa Singida Mashariki, ndugu Tundu Lissu, wakati akitokea Bungeni, tena kwenye makazi yake, ambayo Kwa mujibu wa sheria ni sehemu ya Bunge, ni dharau ya hali ya juu kwa Mhimili huu. Ni tukio linalolenga kuliziba mdomo Bunge. Makala yangu ya Nani alitaka kumwua Tundu Lissu (kwa lugha ya Kiingereza) naiambatanisha katika maelezo yangu haya.

9. Kitendo cha Serikali kutowasilisha 'Taarifa za Utendaji wa Robo Mwaka' kwenye Kamati ya Bunge ya Bajeti kama inavyotakiwa kwa mujibu wa Sheria ya Bajeti ya mwaka 2014 ni dharau kubwa kwa Mhimili wa Bunge. Ni dharau zaidi kwamba Serikali ilileta Muswada wa sheria kuondoa kifungu kinacholazimisha Waziri wa Fedha kutoa Taarifa hizo, na Bunge kupitisha kuwa Sheria, hivyo kuondoa kabisa Uwajibikaji wa kibajeti wa Serikali ndani ya Bunge, hivyo kudunisha hadhi ya bunge.

10. Bajeti ya Bunge kutowekwa kwenye Mfuko wa Bunge kwa mujibu wa sheria, na Spika kutakiwa kuomba vibali vya safari za Wabunge kwa Mkuu wa Tawi la Utendaji (Serikali) ni maelezo tosha kuwa Bunge ni Tawi la Utendaji na sio Mhimili unaojitegemea.

Kuna mihimili mitatu 3 mikuu ya nchi kutokana na katiba ya nchi fulani.Ambayo ni pamoja na serikali,mahakama na bunge na hii zote zinafanya kazi zao pasipo kuingiliana lakini serikali imekuwa ikiingilia bunge pasipo kufata katiba (uthibitisho wa mheshimiwa zitto)

Labda tatizo hili linatokana na KATIBA na nchii hii kwani ni raisi mwenyewe mwenye mamlaka ya kuchagua spika wa bunge pamoja na jaji mkuu wa mahakama na hii inaashiria kwamba kuna muingiliano wa mihimili hii.

WAZO...
KATIBA ya nchi irudiwe upya kwa maana irekebishwe ili kulinda mihimili hii kuingiliana moja kwa nyingine ili kulinda adhabu hizi tuzipatazo kwa sasa

MWISHO...
MANENO ya ZITTO ni sumu kwa viongozi hewa ambao hawafati sheria na katiba yake kwa ujumla

WELL SAID ZITTO
e7330d09592e80b0277ac261b1c59d30.jpg
95e1617189972ea2fe6ab5fdd5218ac6.jpg
 
Mazito ya Zitto hayo tena kazi ipo kwa Kamati na Viongozi wa Serikali
 
Inabidi naye aitwe kwenye kamati ya maadili, akikataa wito apelekwe kwa nguvu na polisi. Hoja za ZZK zinampa wakati mgumu Mwenyekiti wa kamati hiyo kwani akizikubali maana yake ni kweli jamaa wa mjengoni anaelekezwa na wa magogoni
 
Kamchana ndugai labda achukuwe ile fimbo kama wakati wa kampeii alivyomzapa mpinzani wake. Watu wadio na busara hufikiria kutumia nguvu. Serikali hii itaiacha nchi njia panda
 
Hoja nzito zilizoambatana na uthibitisho bayana na maelezo yaliyoshiba.

Naamini kabisa, katika watu waliomuhoji Zitto, hakuna anaefikia IQ yake.

Wakati niko form two, nilifundishwa darasani kuhusu demokrasia na kipengele cha mgawanyiko wa madaraka (separation of power).

Nilifundishwa kua kwa nchi yetu mahakama na bunge havina Uhuru stahiki kutokana na kuingiliwa na serikali kuu.

Sasa inashangaza eti spika wetu wa bunge halijui hili. Anaamuru mbunge akamatwe, then asafirishwe kwa kodi za wananchi kwenda kujibu hoja za kitoto namna hii. PATHETIC!

Msitushangae sisi vijana namna tunavyoichukia nchi na kupoteza uzalendo. Ni kwa sababu ya upuuzi na king'ang'anizi cha wazee wenye tamaa na wasiokua na busara.

My dear Tanzania, I have no single reason to love you!
 
Civics
 
Mbunge wa kigoma mjini Mh.ZUBERI KABWE aliitwa kwenye mahojiano na kamati ya maadili ya bunge kutokana na kauli yake wanaodai ni ya kichochezi "bunge sikuhizi ni idara ya tawi la utawala".ZITTO alifafanua kwa kutoa thibitisho 10 nayo ni kama zifuatazo...

1. Kuzuiwa kwa "Bunge Live" kwa kisingizio cha kupunguza gharama za uendeshaji wa mhimili wa Bunge, wakati Mikutano yote ya mhimili wa Serikali, hasa ya Rais ikirushwa live (mubashara) ni dalili ya wazi ya kufifisha sauti ya Bunge na kupandisha sauti ya serikali. Hata vituo binafsi ambavyo vilipanga kurusha bunge Live bila malipo (na hivyo kutokuwa na gharama) vilizuiwa, lakini vinarusha Live mikutano ya Rais.

2. Kitendo cha Uongozi wa Bunge kurudisha serikalini shilingi Bilioni 6 bila ridhaa ya wabunge kwa kisingizio kwamba zimebaki kutokana na kubana matumizi. Hii ni dalili ya wazi ya Bunge "kujipendekeza" kwa serikali. Wakati Uongozi wa Bunge ukirejesha kiwango hicho cha Fedha, kuna taarifa kwamba kamati nyingi za Bunge zinashindwa kutekeleza wajibu wake kwa sababu ya ukata.

3. Maelekezo ya mhimili wa Serikali kwa mhimili wa Bunge, kupitia maagizo ya Rais Magufuli kwa Spika Ndugai kuwa "Awashughulikie wabunge" (kwa kuwafukuza bungeni) aliowaita "waropokaji" ili waje wazungumze nje ya Bunge na yeye Rais (Serikali) apate nafasi ya kuwashughulikia. Kauli hii ya Rais aliyoitoa wakati akipokea Ripoti ya Prof. Osoro kuhusu Mikataba ya Madini, Juni 12, 2017 inaonyesha picha iliyo dhahiri kuwa Bunge linapokea Maelekezo kutoka Serikalini ya kuwadhibiti wabunge hasa wanaoiwajibisha serikali. Na hatuwahi kuliona Bunge likiyakana maelekezo hayo ya Rais kwa Spika.

4. Kitendo cha Bunge kuhariri hotuba za kambi ya upinzani kwa kushinikiza kuondolewa kwa vipengele vinavyoikosoa Serikali. Mathalani, Wakati wa Bunge la Bajeti, hotuba ya Msemaji wa Kambi ya upinzani wa Wizara ya Mambo ya Ndani, ndugu Godbless Lema, iliamriwa kuondolewa maneno yanayohusu kashfa ya Mkataba wa Lugumi, kumhusisha Rais na kuuzwa kwa nyumba za Serikali, Mauaji ya wanasiasa, pamoja na Bunge kulinda wahalifu.

5. Kauli ya Rais Magufuli ya Novemba 4, 2016 akizungumza na wahariri wa vyombo vya habari kuwa "mzizi wa mhimili wa serikali ni mrefu zaidi kuliko mihimili mingine" mara baada ya kuulizwa juu ya matumizi ya Serikali Nje ya Bajeti iliyoidhinishwa na bunge, unaonyesha dhahiri fikra ya Rais na Serikali yake juu ya ukuu wa mhimili wa Serikali dhidi ya Bunge.

6. Kitendo cha Ripoti ya Kamati ya Bunge ya Tanzanite na Almasi kusomwa nje ya Bunge na kuwasilishwa kwa Waziri Mkuu na Rais bila kuwasilishwa na kujadiliwa Bungeni ili kuwekewa azimio la Bunge. Kitendo hiki kinaifanya Kamati hiyo kuonekana kuwa ya Serikali badala ya Kamati ya Bunge.

7. Kauli ya Rais kuwa Spika alimpigia simu kumuuliza juu wajumbe wa kuwaweka kwenye Kamati za Bunge za Tanzanite na Almasi inaonyesha dhahiri kuwa Spika anafanya kazi kwa maelekezo ya Rais. Na Bunge na Spika hawajawahi kuikana kauli hii ya Rais.

8. Kwa mara ya kwanza kwenye Historia ya Nchi yetu tumeshuhudia Mbunge akishambuliwa kwa risasi wakati Mkutano wa Bunge ukiwa unaendelea. Haijapata kutokea katika historia ya Bunge letu, Wabunge kukamatwa hovyo mbele ya mageti ya Bunge na kusafirishwa usiku usiku bila hata Spika kujulishwa kama taratibu za Mabunge ya Jumuiya ya Madola zinavyotaka. Kitendo cha 'Watu Wasiojulikana' kummiminia risasi zaidi ya thelathini Mbunge wa Singida Mashariki, ndugu Tundu Lissu, wakati akitokea Bungeni, tena kwenye makazi yake, ambayo Kwa mujibu wa sheria ni sehemu ya Bunge, ni dharau ya hali ya juu kwa Mhimili huu. Ni tukio linalolenga kuliziba mdomo Bunge. Makala yangu ya Nani alitaka kumwua Tundu Lissu (kwa lugha ya Kiingereza) naiambatanisha katika maelezo yangu haya.

9. Kitendo cha Serikali kutowasilisha 'Taarifa za Utendaji wa Robo Mwaka' kwenye Kamati ya Bunge ya Bajeti kama inavyotakiwa kwa mujibu wa Sheria ya Bajeti ya mwaka 2014 ni dharau kubwa kwa Mhimili wa Bunge. Ni dharau zaidi kwamba Serikali ilileta Muswada wa sheria kuondoa kifungu kinacholazimisha Waziri wa Fedha kutoa Taarifa hizo, na Bunge kupitisha kuwa Sheria, hivyo kuondoa kabisa Uwajibikaji wa kibajeti wa Serikali ndani ya Bunge, hivyo kudunisha hadhi ya bunge.

10. Bajeti ya Bunge kutowekwa kwenye Mfuko wa Bunge kwa mujibu wa sheria, na Spika kutakiwa kuomba vibali vya safari za Wabunge kwa Mkuu wa Tawi la Utendaji (Serikali) ni maelezo tosha kuwa Bunge ni Tawi la Utendaji na sio Mhimili unaojitegemea.

Kuna mihimili mitatu 3 mikuu ya nchi kutokana na katiba ya nchi fulani.Ambayo ni pamoja na serikali,mahakama na bunge na hii zote zinafanya kazi zao pasipo kuingiliana lakini serikali imekuwa ikiingilia bunge pasipo kufata katiba (uthibitisho wa mheshimiwa zitto)

Labda tatizo hili linatokana na KATIBA na nchii hii kwani ni raisi mwenyewe mwenye mamlaka ya kuchagua spika wa bunge pamoja na jaji mkuu wa mahakama na hii inaashiria kwamba kuna muingiliano wa mihimili hii.

WAZO...
KATIBA ya nchi irudiwe upya kwa maana irekebishwe ili kulinda mihimili hii kuingiliana moja kwa nyingine ili kulinda adhabu hizi tuzipatazo kwa sasa

MWISHO...
MANENO ya ZITTO ni sumu kwa viongozi hewa ambao hawafati sheria na katiba yake kwa ujumla

WELL SAID ZITTO
e7330d09592e80b0277ac261b1c59d30.jpg
95e1617189972ea2fe6ab5fdd5218ac6.jpg
 
Hizi hoja ni ninyi tu mnaziona zianafaa na zina mashiko.
Ngoja wakulu wajibu ndio mtakapochukia na kupasuka kichwa.
 
Na ccm wanavowaogopa wapinzani wakiongozwa n mwenyekiti wao sidhani km watakuja kumuita kumhoji tena iwapo akitoa kauli yoyote.....huwezi kuwa ccm na ukawa na akili ya kuwatetea watz
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom