GE2025 Manara: Nitamfikia kila mpiga kura wa Kata ya Kariakoo

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

Mkalukungone Mwamba

JF-Expert Member
Joined
Aug 29, 2022
Posts
2,436
Reaction score
5,234
Mgombea Udiwani wa Kata ya Kariakoo kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Haji Sunday Manara, ameahidi kuwafikia wapiga kura wote wa kata hiyo ili kuwaomba kura, akisisitiza kuwa bado ana nguvu na ari ya kufanya kazi hiyo kikamilifu.

Soma Pia: Mgombea Udiwani kata ya Kariakoo Haji Manara akiomba kura ndani ya Daladala

Manara alitoa kauli hiyo wakati wa kikao cha ndani cha Kamati ya Siasa ya CCM Kata ya Kariakoo, kilichoitishwa kwa lengo la kujadili na kupanga mikakati ya kampeni kwa ajili ya kuwaombea kura wagombea wa chama hicho. Kikao hicho kilijadili mikakati ya kumsaidia mgombea urais wa CCM, Dkt. Samia Suluhu Hassan, pamoja na mgombea ubunge wa Jimbo la Ilala, Mussa Azzan Zungu.

Your browser is not able to display this video.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…