nyehura
Member
- Jun 4, 2022
- 6
- 15
Haji Manara alifungiwa mwaka 1 na faini ya shilingi Milioni 9 mwezi April 2017 baada ya kukutwa na Makosa 3 ambayo yaliwekwa wazi na Kamati ya Maadili ya TFF.
1) Kuituhumu na Kuidhalilisha TFF na Viongozi wake kwa kutoa maneno yasiyo na Staha.
2) Kueneza Chuki za Ukabila. 3) Kuingilia Utendaji wa TFF.
Kosa la kwanza alihukumiwa kwa mujibu wa kanuni 41 Kifungu cha 9 ambapo alihukumiwa kulipa milioni 1. Kosa la pili alihukumiwa kwa kanuni ya 53 kifungu cha 1 & 2.
Kutokana na kifungu hicho, alihukumiwa kifungo cha miezi 3 na faina ya shilingi milioni 3. Kosa la tatu alihukumiwa kwa kanuni ya 1 & 2 inayohusu Maadili ya TFF.
Haji alitakiwa ahukumiwe kifungo cha miaka 7 na faini ya Milioni 5 kutokana na kukutwa na hatia kwenye kosa lake la 3 la Kuingilia Utendaji wa TFF.
Ila kutokana na kwamba hayo yalikuwa makosa yake ya mara ya kwanza, Kamati ilitumia mamlaka yake kwa kumpunguzia adhabu hadi miezi 12 na faini ya milioni 5.
Adhabu hizo ziliunganishwa , hivyo alitakiwa kutumikia kifungo cha mwaka mmoja na kulipa faini ya shilingi milioni 9 Lakini Uongozi wa Karia ulimsamehe adhabu hizo zote.
Septemba 2020, Haji alitozwa faini ya shilingi milioni 5 baada ya kukutwa na kosa la kuingilia majukumu ya Kamati ya Katiba, Sheria na Hadhi ya Wachezaji.
Haji alipewa na onyo la kukaa miaka 2 bila kufanya kosa lolote la kimaadili. Julai 2022 Haji alikutwa na hatia kwa makosa mawili 1) Kumtishia 2) kumdhalilisha Rais wa TFF.
Katibu wa Kamati ya Maadili ya TFF, Walter Lungu amesema Haji alimwambia Rais wa TFF, Wallace Karia "Niondolee Upuuzi wako" Aisee ni makosa sana.
Pia alimwambia Rais Karia "Unanifuata fuata sana na hii ni mara ya 3, sikuogopi kwa lolote na nina uwezo wa kukufanya lolote na huna uwezo wa kunifanya lolote".
This time amefungiwa miaka 2 kutojihusisha na soka ndani na nje ya mipaka ya Tanzania na faini ya milioni 20.