Huyu Manager wa Tanroads mkoa wa Arusha sijui anafikiri mkoa wake wote una barabara za lami? Barabara ya kutoka Karatu mkoani Arusha kuelekea Mbulu mkoa wa Manyara ni mbaya sana ni mashimo matupu na rasta kilichobaki ni wajawazito kujifungua njiani kabla ya muda wao kufika. Huyu jamaa aitwaye Eng. Johnny Kalupale amejikalia zake pale mjini Arusha anakula bata wakati mwenzake wa mkoa wa Manyara Eng. Bashir Rwesingisa anafanya periodic maintenance kwa mara ya tatu sasa ndani ya miezi kama sita. Hili utalishuhudia ukifika tu mpakani mwa mkoa wa Arusha na Manyara eneo la Kilimapunda. Upande wa Mkoa wa Manyara hata km ni ya vumbi ni nzuri sana, upande wa mkoa wa Arusha Kilomita km 53 ni balaa sijawahi sehemu yoyote ktk hii Tanzania. Mh. Rais huyu Manager wa mkoa wa Arusha anasubiri nini ofisini? Pongezi zake Eng. Bashir Rwesingisa kwa kazi nzuri