Man United yakataa mabilioni kwa Januzaj

Man United yakataa mabilioni kwa Januzaj

Mad Scientist

JF-Expert Member
Joined
Jul 27, 2013
Posts
215
Reaction score
77
HATUTAKI, na tena hatutaki hata
kusikia. Na ikiwezekana msirudi tena.
Ndivyo ambavyo mapovu yamewatoka
mdomoni watu wa Manchester United
baada ya PSG kurudi mezani juzi
Jumapili na ofa ya kumtaka kinda wao
mahiri, Adnan Januzaj.
PSG wamekuwa wakitokwa udenda kwa
kinda huyo mwenye asili ya Albania
aliyezaliwa Ubelgiji miaka 18 iliyopita na
hawajali kama aliingia mkataba mpya
wa kuichezea Man United mwishoni mwa
msimu uliopita.
Hata hivyo, kocha David Moyes
amekataa ofa hiyo ya PSG
inayodhaniwa kuanzia Pauni 25 milioni
na kuendelea huku wakisisitiza kwamba
hawana mpango hata wa kukaa chini
na kuzungumza na matajiri hao wa
mafuta kutoka Paris.
Man United imempatia mkataba mrefu
wa miaka mitano Januzaj Oktoba mwaka
jana baada ya kugundulika kuwa
huenda mchezaji huyo angekuwa huru
na kuondoka Mei mwaka huu mara
baada ya msimu kumalizika.
Kabla na baada ya kusaini mkataba
huo, Januzaj ameibuka kuwa miongoni
mwa wachezaji wachache mahiri katika
kikosi cha Man United ambacho msimu
huu kimekuwa kikisuasua ndani ya
uwanja.
Kwa mujibu wa gazeti la Guardian la
Uingereza, Januzaj angeingiza kiasi
kikubwa cha pesa kama angeamua
kukubali kwenda PSG, lakini mwenyewe
ameamua kubaki Man United licha ya
timu hiyo kuwa katika hatari ya kukosa
kucheza Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu
ujao.
Katika mkataba wake wa awali nyota
huyo alikuwa akiingiza kiasi cha Pauni
1,000 tu kwa wiki kutokana na kuwa
kinda mwanafunzi, lakini mkataba wake
wa sasa unamwingizia kiasi cha Pauni
30,000 kwa wiki.
Akiwa na PSG angeweza kuingiza kiasi
cha zaidi ya Pauni 80,000 kwa wiki,
lakini staa huyo ameamua kubaki Man
United na kuendelea kujifunza zaidi
wakati huu kocha Moyes akimwamini na
kumpanga mara nyingi zaidi katika safu
ya ushambuliaji.
Wakati huohuo pia, PSG pia imekataliwa
katika ofa yao ya Pauni 14 milioni kwa
ajili ya kumchukua kiungo mahiri wa
Newcastle United, Yohan Cabaye
ambaye amekuwa akisakwa kwa muda
mrefu na kocha Laurent Blanc.
Newcastle inaamini kuwa staa huyo
Mfaransa ana thamani ya Pauni 25
milioni na inadaiwa kuwa hata Man
United wameanza kumtolea macho
Cabaye.
 
Hy itakuwa nzuri sana , kwa mtizamo wangu huyu januzaj baadae anaweza akawapa hela nyingi man u zaidi ya hy,, huyu dribbling boy anajua mpira, wamwache tu huenda akawa CR mpya baadae.
 
Hy itakuwa nzuri sana , kwa mtizamo wangu huyu januzaj baadae anaweza akawapa hela nyingi man u zaidi ya hy,, huyu dribbling boy anajua mpira, wamwache tu huenda akawa CR mpya baadae.

Hyo itategemea na nafasi na fursa atakayopewa.
 
Back
Top Bottom