Mamlaka ya maji Morogoro Wizi Mtupu!!

proisra

JF-Expert Member
Jun 14, 2012
213
158
Hii Mamlaka ya Maji Morogoro (MORUMWASA) inafaa ivunjwe mara moja kwa sababu inachangia wananchi kukumbwa na magonjwa ya mlipuko wanapojikuta wanatumia maji yasiyofaa kwa binadamu.

Uzembe huu umejitokeza zaidi kipindi hiki cha nane-nane, ambapo maji yote yameelekezwa kumwagilia miche ya viwanja hivi. Maeneo ya Bigwa, Kola B, Nanenane, Msufini, Kihonda n.k. yalikatiwa maji kwa zaidi ya mwezi sasa. Mbaya zaidi, mita hazisomwi kuonesha kwamba huyu mteja kwa mwezi mzima hajapata maji, badala yake wanataka ulipie gharama ya mwezi wote, hata kama hukupata huduma hii. Wafanyakazi hawawajibiki, pale ambapo upande mmoja wa mtaa (mfano Kola B na Njia panda DSM) wanapopatiwa mgawo wa maji kwa wiki mara moja au mbili huku upande wa pili wakiambulia patupu. Hii kubweteka kwa watumishi hawa inatokana na sababu hii ya kuleta bili za mwezi bila kuzingatia upatikanaji wa huduma husika. Mishahara yao ipo pale pale, ndiyo maana wanajisahau, na kubweteka.

Tunaomba EWURA na wahusika wengineo waingilie kati aina hii ya wizi, ili utaratibu wa Lipia maji kadiri unavyotumia uanzishwe Morogoro kama ilivyo kwa wateja wa umeme wanaotumia LUKU.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom